Siha Njema podcast artwork

PODCAST · health

Siha Njema

Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.

Publisher-supplied feed metadata · PodParley refreshed Sep 25, 2026 · Source feed

  1. 24

    Kwa nini bima ya afya ya msafiri ni sharti muhimu kwa mataifa ya Afrika

    Umuhimu wa bima ya afya kwa wasafiri ni pamoja na kupunguza gharama kwa taifa mwenyeji haswa wakati huu nchi nyingi hususan za Afrika zinashuhudia ongezeko la milipuko wa magonjwa ya milipuko Sharti hilo pia linatoa fursa kwa nchi kuboresha mifumo ya afya ili kukidhi mahitaji ya wasafiri wanaohitaji huduma za afya kwa nchi wanazozitembelea.

  2. 23

    Unaweza kuendelea kunyonyesha hata baada ya kutenganishwa kwa muda na mwanao

    Imani kuwa mama na mtoto wanapotenganishwa inaweza kuathiri ubora wa maziwa ya mama inapotosha. Watalaam wanasisitiza maziwa ya mama hayawezi kuharibika kwenye titi. Aidha kunyonyesha kwa uaminifu kunaweza kukuepusha na saratani na mbinu pia ya kupanga uzazi.

  3. 22

    Kwa nini watalaam wanahoji maumivu makali wakati wa hedhi si kawaida

    Maumivu wakati msichana au mwanamke anapokuwa kwenye siku zake za hedhi, yanaweza kuwa ya kawaida ila maumivu haya yanapomfanya kushindwa na shughuli za kawaida si kawaida Dkt Dominic Osiemo anasema maumivu haya makali yanaweza kuwa dalili za baadhi ya changamoto za kiafya kama vile Uvimbe au ugonjwa wa Endometriosis.

  4. 21

    Changamoto ya wanaume na wanawake kukosa hamu ya tendo la ndoa

    Raia mmoja wa Kenya amefika kwenye bunge la kitaifa nchini Kenya akitaka swala la wanaume na wanawake kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa kuorodheshwa kuwa ulemavu Kwa mujibu wa daktari Dominic Osiemo ,tatizo hilo linachangiwa na maswala kadhaa yakiwemo matumizi ya dawa za kisukari ,shinikizo la damu na msongo wa mawazo.

  5. 20

    Visa vya kung'atwa na Nyoka vyaongezeka kaunti ya Turkana Nchini Kenya

    Kaunti ya Turkana inaongoza nchini Kenya kwa visa vya watu kung'atwa na nyoka. Wataalamu wa afya wanasema mabadiliko ya tabianchi, joto kali na changamoto za upatikanaji wa huduma za afya vinaongeza hatari kwa wakazi wa maeneo mengi ya kaunti hiyo,huku shirika la afya duniani WHO likisema visa vya kuumwa na nyoka vinapuuzwa wakati huu karibia watu 32000 wakifariki kila mwaka  kutokana na sumu ya nyoka.Katika makala haya ya siha njema tunaangazia kijiji cha Kapua kwenye kaunti hiyo .

  6. 19

    Mashirika ya kiraia Afrika yaanza kampeni dhidi ya madeni ya umma

    Mashirika ya kiraia yanasema nchi za Afrika zinalipa deni na kuachwa  na kiasi kidogo cha pesa kuendesha shughuli muhimu za serikali ,sekta ya afya ikiathirika zaidi Mashirika haya yanataka umoja wa Afrika kuja na jopo ambalo litakuwa linaangazia  maswala yote kuhusu mikopo ili kupunguza dhulma kwa nchi zinazoendelea

  7. 18

    Kampeni kuhakikisha vyakula vilivyosindikwa vina maandishi ya kuonya

    Tafiti kadhaa za kiafya zimebainisha magonjwa mengi yasiyoambukizwa yana uhusiano mkubwa na vyakula vilivyosindikwa  na hali ya watu kukosa kuzingatia mazoezi  ya kila mara. Kenya ikiwa taifa la kwanza Afrika Mashariki kupitisha  mwongozo unaotoa maelekezo kuhusu viwango vya  madini ambavyo  vyakula au vinywaji  vinavyouzwa vinafaa kukidhii  au kwa lugha ya kiingereza Kenya Nutrient Profile Model,sasa ipo mbioni kuja na sheria kushinikiza maandishi ya kuonya kuhusu vyakula venye mafuta ,sukari na chumvi nyingi kupachikwa kwenye bidhaa za vyakula na vinywaji

  8. 17

    Kwa nini ni muhimu wanaume kuzingatia afya zao haswa afya ya akili

    Mwezi Juni ni mwezi wa kutoa uhamasisho kuhusu afya ya akili miongoni mwa wanaume ,swala la afya ambalo hupuuzwa mno Daktari Dominic Osiemo anasema wanaume wana haki wa kuonesha hisia ,kueleza maumivu  yao na kutaka kuskizwa. Na wanapofanya hivyo wanalinda afya zao za akili. Anaonya wanaume wengi wanakuwa hatarini kwa sababu wanajaribu kudhihirishia jamii kuwa wao ni imara siku zote. Baadhi ya vipimo muhimu kwa wanaume ni kipimo cha kiwango cha sukari ,kipimo cha tezi dume na shinikizo la damu.

  9. 16

    Shule ya Mali jijini Nairobi inavyowasaidia watoto wenye Austism pamoja na wazazi

    Katika mkakati wa kupunguza unyanyapaa kwa wazazi wanaowalea watoto wenye Autism shule ya Mali inatoa tiba nasaha  na elimu kwa pamoja ikizingatia pia mahitaji ya wazazi wao ambao mara nyingi wanahitaji pia matunzo

  10. 15

    Shinikizo kutaka mataifa kuja na sera endelevu na salama za uchukuzi

    Shinikizo zinazidi kutolewa kwa mataifa ya Afrika kukumbatia sera za uchukuzi zilizo salama na endelevu ili kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na barabara na madhara ya ajali za barabara kwa jamii. Katika  kongamano la kujadili mpango huo wa usalama ulio endelevu ,wadau wamesikitika vifo vya barabarani bado vinaripotiwa miongoni mwa watembea miguu na waendesha pikipiki. Katika makala ya Siha Njema wiki hii tunajadili kwa nini swala hili ni muhimu kwa ustawi wa jamii.

  11. 14

    Majanga yanaweza kusababisha matatizo ya afya ya akili miongoni mwa watoto

    Mataifa ya Afrika yameshuhudia mafuriko katika miaka ya hivi karibuni ,hali ambayo imesababisha wananchi wengi kulazimika kuhama makazi yao Nchini Kenya ,ukanda wa magharibi ,katika eneo la Busia,mafuriko hayo yamevuruga kalenda za wanafunzi wa shule ,watoto wengi wakishindwa kuendelea na shule au kukubaliana na msongamano kwenye shule chache ambazo ziko maeneo salama Hali hii imewasababisha changamoto za afya ya akili anavyoeleza mwaandishi wetu Petronila Ogalo.

  12. 13

    Mwendelezo wa mlipuko wa Ebola DRC na namna wenyeji wanavyojikinga

    Watu 220 wamefariki kwenye mlipuko wa Ebola unaohusishwa na virusi adimu vya Bundibugyo huku wengine zaidi ya 1000 wakiwa wameambukizwa Mlipuko huu hatari umesababisha baadhi ya mataifa kufunga mipaka yake na kuweka masharti magumu ya tahadhari

  13. 12

    Kwenye kapu la sekta ya afya kufuatia kongamano la Africa Forward

    Baadhi ya makubaliano yalitotangazwa na Ufaransa baada ya siku mbili ya kongamano la  Africa Forward ni ufadhili kwa uzalishaji wa dawa na chanjo hapa barani Afrika. Shirika la Unitaid  pia lenye ushirikiano na Ufaransa lilitangaza kuratibu mchakato wa kuzalishwa dawa mpya ya kuzuia virusi vya HIV ,Lenacapavir kuzalishwa Afrika Kusini. Na kwenye viungo vingine vilivyosheheni majadiliano ya kuimarisha mifumo ya afya Afrika ni kilimo endelevu .

  14. 11

    Mashirika ya kiraia Afrika yanataka nchi za Afrika kuwa na taratibu za pamoja kudhibiti magonjwa

    Taratibu hizo za pamoja yatahakikisha kuwa nchi za Afrika zinaweka bajeti kwenye sera ya uchumi na kuipa kipau mbele ufadhili wa afya

  15. 10

    Watalaam wasisitiza uwekezaji wa utafiti wa DNA barani Afrika

    Utafiti unaoangazia vinasaba katika ukanda wa Afrika unaweza kuwa jawabu kwa ubainishaji potovu,gharama ya juu ya matibabu na usugu wa vimelea .  Kwa kuanzia , Mashirika matatu ya Afrika ya kitafiti  yametangaza mkataba wa dola milioni 3 nukta 5 ambao utawekezwa  kwenye utafiti  huu wa DNA  barani . Mashirika haya yakiwa ni Biolinx Africa,  YTO Foundation  yenye makao Ivory Coast na  Nextgen Molecular Lab nchini Kenya.

  16. 9

    Mpango wa kuongeza ujuzi wa wahudumu wa afya kwa kutumia teknolojia

    Ufadhili wa afya ukanda wa Afrika umezidi kupungua tangu kusitishwa kwa ufadhili mkubwa wa kigeni Pengo hilo linamanisha serikali nyingi hazina uwezo wa kifedha wa kutosha kuendelea kutoa mafunzo endelevu ya wahudumu wa afya. Katika kujaribu kutatua changamoto hii ,mpango wa ECHO unaowasaidia wahudumu wa afya kujifunza wakati wanapoendelea kuwahudumia wagonjwa ,umekuja kuleta matumaini.

  17. 8

    Mataifa ya Afrika mbioni kuboresha mkataba wa kupambana na majanga

    WHO ilitoa nafasi zaidi kwa mataifa ya ulimwengu kujadililiana zaidi kuhusu vipengee muhimu kwenye mkataba wa kukabiliana na majanga ya kidunia Vipengee hivyo ni pamoja namna mataifa yanaweza kunufaika kutokana na mchango wao kwenye tafiti za kisayansi ,vimelea vinavyotoka kwenye mataifa yao na usawa wakati wa usambazaji wa chanjo au dawa

  18. 7

    Miaka mitatu tangu Sudan kuingia kwenye mzozo huduma za afya zimedorora

    Asilimia 37 ya vituo vya afya nchini Sudan vimeharibiwa wakati wa mapigano na haviwezi kutoa huduma za afya Shirika la madaktari wasio na mipaka,MSF limekuwa likiwahudumia wagonjwa wenye majeraha ,waathiriwa wa magonjwa ya milipuko na waathiriwa wa ubakaji. Hali ya usalama imeilazimu  MSF kusitisha huduma katika maeneo kadhaa baada ya kushuhudiwa mashambulizi ya moja kwa moja kwenye vituo vya afya ,vituo hivyo kuporwa na uhaba wa bidhaa za kimatibabu unaohusishwa na vikwazo vya usafiri.

  19. 6

    Kliniki tembezi za figo zinavyowasaidia wagonjwa wa figo nchini Kenya

    Idadi ya wagonjwa wa figo imekuwa ikiongezeka kutokana na kuongezeka pia kwa magonjwa yasiyoambukiza kama vile Kisukari.

  20. 5

    Magonjwa ya Autoimune yana uwezo kukusababishia magonjwa mengine zaidi

    Magonjwa yanayoshambulia kinga yanapompata mtu ,huendelea kusambaa ,kudhuru kingamwili na  kumweka hatarini mgonjwa kiasi cha kuwa mgonjwa anaweza kupatwa na magonjwa zaidi ya moja ya aina hiyo. Elwyn Chebet aligunduliwa na Lupus na baadaye akajikuta anapambana na magonjwa zaidi ya tano aina ya Autoimmune. Mwezi Machi ambapo ulimwengu huelekeza kurunzi kwenye magonjwa ya mfumo wa kinga au Autoimmune,watalaam wanasikitika kuhusu ufahamu mdogo kuhusu magonjwa haya. Wagonjwa wengi huwa na dalili za kukanganya na ubainishaji wa magonjwa haya unaweza kuchukua muda mrefu na kugharimu kiasi kikubwa cha pesa. Na kwa kuwa vyanzo vya magonjwa haya huwa haviko wazi matibabu yake huwa yenye mtihani mkubwa.Watalaam wengi hujaribu kutibu dalili bila kushughulikia chanzo cha ugonjwa wenyewe. Katika makala haya tumezungumza na Elwyn Chebet ambaye ni shujaa na mwanaharakati wa ugonjwa wa Lupus ambao huathiri viungo kadhaa mwilini na hata ngozi. Katika simulizi yake ,anaeleza kuwa kutokana na kinga dhaifu magonjwa tegemezi kama mafua,Malaria na Menegitisi yanaweza kuhatarisha maisha yake hivyo huhitajika kupata chanzo ya mapema dhidi ya magonjwa haya.

  21. 4

    Visa vingi vya TB Afrika bado vinapatikana miongoni mwa vijana hasa wanaume

    Watalaam wanasema vijana wengi hufikia kwenye maduka ya kuuza dawa kupata huduma za afya baadala ya kufika hospitali kufanyiwa vipimo Unyanyapaa pia inachangia wanaume au vijana kuwa na ari ya kwenda kupata huduma za afya haswa za TB.

  22. 3

    Nini magonjwa yanayoathiri kinga mwili au Autoimmune

    Unapopata magonjwa ambayo yanaathiri kinga ya mwili wako,ina maana kuwa kinga yako inaweka mifumo yote ya mwili kwenye hatari. Unaweza kujikuta unapata magonjwa kama Lupus,ugonjwa wa Tezi Koo au Mifupo yako kuwa nyepesi kiasi cha kuvunjika kwa urahisi. Ubainishaji wa magonjwa haya unahitaji subira na ufuatialiaji wa karibu ili kuelewa kila dalili anayoonesha mgonjwa .Gharama yake basi inamanisha ni ya juu na huhitaji muda mrefu.

  23. 2

    Kampeni ya kumaliza unyanyapaa wa siku za hedhi kwa kushirikisha wanaume

    Siku za hedhi huchukuliwa kuwa swala la wanawake na halifai kuzungumzwa hadharani kwa jamii nyingi .Hali hii imesababisha wanawake na wasichana kupitia unyanyapaa ijapokuwa hili ni swala la haki ya uzazi

  24. 1

    Madhara ya afya ya akili yanayotokana na matumizi ya kupitiliza ya simu

    Ripoti ya afya akili  duniani ,inaonya kuhusu madhara yanayotokana na matumizi ya simu za mkononi miongoni mwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 na 34 Katika mataifa ya Afrika ambapo matumizi ya simu hizi huanza kwa kuchelewa ,vijana walionekana kuwa afadhali ikilinganishwa na mataifa kama Finland ambapo watoto huanza kutumia simu katika umri mdogo mno.   Katika mataifa yaliyozingatia maswala ya dini na muunganiko wa familia na jamii walionekana pia kuwa na ahueni.

Type above to search every episode's transcript for a word or phrase. Matches are scoped to this podcast.

Searching…

We're indexing this podcast's transcripts for the first time — this can take a minute or two. We'll show results as soon as they're ready.

No matches for "" in this podcast's transcripts.

Showing of matches

TOPICS IN THIS SHOW

Click any topic to search every transcript on PodParley for moments someone mentioned it.

Loading reviews...

ABOUT THIS SHOW

Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.

HOSTED BY

RFI Kiswahili

Produced by France Médias Monde

CATEGORIES

Frequently Asked Questions

How many episodes does Siha Njema have?

Siha Njema currently has 24 episodes available on PodParley. New episodes are automatically indexed when they're published to the podcast feed.

What is Siha Njema about?

Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao...

How often does Siha Njema release new episodes?

Siha Njema has 24 episodes. Check the episode list to see recent publication dates and frequency.

Where can I listen to Siha Njema?

You can listen to Siha Njema on PodParley by clicking any episode. We provide an embedded audio player for direct listening, and you can also subscribe via your preferred podcast app using the RSS feed.

Who hosts Siha Njema?

Siha Njema is created and hosted by RFI Kiswahili.
URL copied to clipboard!