PODCAST · government
MAELEZO PODCASTS
by Tanzania Information Services Department, Habari-MAELEZO
Sikiliza MAELEZO PODCASTS (Podcasts za Kiswahili kutoka Idara ya Habari MAELEZO, Tanzania) kupata taarifa na matukio mbalimbali nchini Tanzania. Idara ya Habari (MAELEZO) ipo chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ikiwa na jukumu la kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa Sera, mipango na miradi ya maendeleo vinavyotekelezwa na Serikali kwa wananchi, kusimamia vyombo vya habari hasa magazeti na machapisho na kuishauri Serikali juu ya Sera na Sheria za habari.
-
0
Fursa, Ushirikiano kati ya Algeria na Tanzania: Balozi Matinyi
Send us Fan MailMheshimiwa Balozi Mobhare Matinyi akizungumza mara baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho wa kibalozi kwa Mheshimiwa Abdelmadjid Tebboune, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, katika hafla iliyofanyika kwenye Ikulu ya Algiers tarehe 10 Juni, 2026. Balozi Mobhare Matinyi anayeiwakilisha Tanzania nchini Algeria, ametoa wito kwa Watanzania kutumia fursa za ushirikiano mzuri baina ya nchi hizi kufaidika katika nyanja mbalimbali.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali
-
-1
Balozi Kombo Aeleza Umuhimu wa Ziara ya Rais Samia katika Kuimarisha Mahusiano ya Tanzania na Urusi
Send us Fan MailMkutano na Waandishi wa Habari kuhusu ziara ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Urusi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, tarehe 7 Juni, 2026.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali
-
-2
Miaka 10 ya BMH: Jinsi Hospitali ya Benjamin Mkapa Ilivyobadilisha Huduma za Kibingwa Tanzania
Send us Fan MailHospitali ya Benjamin Mkapa ni hospitali ya rufaa ya kanda iliyopo jijini Dodoma, iliyoanzishwa kwa lengo la kutoa huduma za kibingwa ambazo kwa sasa zipo 20 na ubingwa bobezi zipo 17 kwa wananchi wa Tanzania na nchi jirani. Tangu kuanza kutoa huduma zake, hospitali hiyo imeendelea kukua kwa kasi na kuwa miongoni mwa vituo vinavyoongoza nchini katika huduma za matibabu ya moyo, figo, saratani, upasuaji mkubwa pamoja na huduma za kisasa za uchujaji damu na upandikizaji wa figo. Aidha, hospitali imejizatiti katika kukuza utalii wa matibabu na mafunzo ya kitaalamu, huku ikitoa huduma kwa mamilioni ya wananchi kila mwaka. Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali
-
-3
Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 (Mei 4, 2026)
Send us Fan MailWaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, akiwasilisha makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Mei 4, 2026, bungeni, jijini Dodoma.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali
-
-4
Hotuba ya Mhe. Rais Samia na Mhe. Rais, Paul Kagame, Mei 03, 2026
Send us Fan MailRais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame, amefanya ziara ya siku moja nchini Tanzania, akizungumza na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu ushirikiano na kukuza uchumi wa pande zote, Mei 3, 2026.Viongozi hawa walikubaliana kuendelea kukuza biashara na uwekezaji kwa kuondoa vikwazo vya kikodi, ili kunufaika na masoko ya kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA).Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali
-
-5
Hotuba ya Rais, Dkt. Samia Kwenye Kongamano la Biashara Baina ya Tanzania na Kenya, Mei 4, 2026
Send us Fan MailRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na Kenya (Tanzania & Kenya Business Forum 2026), tarehe 04 Mei, 2026, JNICC, jijini Dar es Salaam ambapo kongamano hili lilihudhuriwa pia na Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. William Samoei Ruto.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali
-
-6
Elimu kuhusu ugonjwa wa Seli Mundu na Dkt. Catherine Mhando
Send us Fan MailPata ufahamu sahihi kuhusu chanzo, dalili, matibabu pamoja na kinga ya ugonjwa wa Seli Mundu (Sickle Cell) na Dkt. Catherine Mhando wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali
-
-7
Buriani Benjamin mkapa (Julai 25, 2020)
Send us Fan MailSupport the showMsemaji Mkuu wa Serikali
-
-8
Elimu kwa umma kuhusu zoezi la SENSA YA WATU NA MAKAZI (2022)
Send us Fan MailMatokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni kwa ajili ya mipango jumuishi na maendeleo endelevu ya nchi na yataongeza uwazi katika kugawa rasilimali zilizopo kuendana na uwiano wa idadi ya watu katika ngazi zote za utawala. Halikadhalika matokeo yatatumika na Serikali na wadau wengine katika kufuatilia na kutathmini mipango mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikijumuisha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Dira ya Zanzibar 2050, Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Mwaka 2021/22 - 2025/26 na Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar (2021/22 - 2025/26), Dira ya Maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2050 na Ajenda ya Maendeleo ya Afrika 2063. Taarifa hizi zitaipima Tanzania katika hatua iliyofikia kwenye utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu; Mpango ambao unalenga kuleta usawa na kutokomeza umaskini wa aina zote ukiwemo umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2030 kwa kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeachwa nyuma.Support the showMsemaji Mkuu wa Serikali
We're indexing this podcast's transcripts for the first time — this can take a minute or two. We'll show results as soon as they're ready.
No matches for "" in this podcast's transcripts.
No topics indexed yet for this podcast.
Loading reviews...
ABOUT THIS SHOW
Sikiliza MAELEZO PODCASTS (Podcasts za Kiswahili kutoka Idara ya Habari MAELEZO, Tanzania) kupata taarifa na matukio mbalimbali nchini Tanzania. Idara ya Habari (MAELEZO) ipo chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ikiwa na jukumu la kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa Sera, mipango na miradi ya maendeleo vinavyotekelezwa na Serikali kwa wananchi, kusimamia vyombo vya habari hasa magazeti na machapisho na kuishauri Serikali juu ya Sera na Sheria za habari.
HOSTED BY
Tanzania Information Services Department, Habari-MAELEZO
CATEGORIES
Loading similar podcasts...