PODCAST · news
Tenda Radio TZ Podcast
by Tenda Radio TZ
TENDA RADIO ni ‘podcast radio’ iliyojikita katika kuwafahamisha, kuwaelimisha na kuwahamasisha wasikilizaji kuhusu fursa za tenda za Serikali, na jinsi ya kupata fursa ya kujipatia fedha za ununuzi wa umma kupitia Mfumo wa NeST. Pia, maudhui haya yanaruka kupitia radio washirika wetu nchini Tanzania ikiwemo Radio Free Afrika, C-FM (Dodoma), A FM (Dodoma), Uyui FM (Tabora), Jembe FM (Mwanza) na nyingine. Imepewa nguvu na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).
-
8
MABILIONI YANAVYOTOLEWA KWA WATU WENYE ULEMAVU KUPITIA MFUMO WA NeST
Zaidi Shilingi Trilioni 5 ya Tenda za serikali iliyotengwa kwa ajili ya makundi maalum yaani vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu inakusubiri wewe?Sikiliza msimu mpya wa Tenda Radio. Jumatano hii tukupe code ya kupata sehemu ya fedha hizo kwa kufanya kazi na serikali kupitia ununuzi wa umma kwenye mfumo wa NeST kwa watu wenye ulemavu.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uthibiti wa Ununuzi wa Umma Bw.Denis Simba atafunguka kuhusu jinsi ambavyo fursa za Tenda zimeongezeka kwa ajili ya Makundi Maalum kwa mwaka wa fedha 2025/2026Mheshimiwa Ridhiwani Jakaya Kikwete,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) atasikika. Wabunge wanaowakilisha watu wenye ulemavu Bungeni nao watazungumza bila kusahau watu wenye ulemavu waliopata Tenda za Serikali nao watueleza wao wamewezaje.
-
7
FURSA ZA SHERIA MPYA YA UNUNUZI WA UMMA, NEEMA NA ADHABU
Tenda Radio imefanya mahojiano maalum na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Wakili Msomi Paul T. Kadushi, amefunguka fursa zinazopatikana kwenye sheria mpya ya ununuzi wa umma ya Tanzania. Sheria hii ina fursa nyingi na neema kwa watanzania, lakini pia ameeleza adhabu kwa watakaoikiuka. Hapa kamata fursa za asilimia 70% ya Bajeti ya Serikali ambayo mwaka huu wa fedha inasoma Sh. 49.3 Trilioni
-
6
NeST ya MAMA SAMIA
Artist: Amini Song Writer: Joseph MuhoziProducer: C9
-
5
JINSI YA KUPATA KIASI CHA BAJETI MPYA YA SERIKALI KUPITIA MFUMO WA NeST, TUKO BUNGENI
Tenda Radio Sehemu ya 5 inazungumzia jinsi ambavyo wazabuni wa Tanzania wamepewa upendeleo maalum kwenye sheria mpya, na jinsi ambavyo wanaweza kupata sehemu ya Bajeti ya Serikali iliyotangazwa bungeni (2024/25). Ndani, utamsikia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Eliakim Maswi na kiundani tunazungumza na wabunge wawili wa Bunge la Jamhuri.
-
4
Jinsi watumiaji wanavyokuwa salama kwenye Mfumo wa NeST
Hii ni sehemu ya Nne ya Tenda Radio, ambapo pamoja na mambo mengine, tumezungumzia usalama wa watumiaji katika Mfumo wa NeST. Tumezungumza na Mkurugenzi wa Mifumo ya TEHAMA ambaye pia ni Meneja Mradi wa Ujenzi wa Mfumo wa NeST, Bw. Michael Moshiro.
-
3
FURSA YA ZAIDI YA SH. 104 BILIONI, NA JINSI YA KUPATA SEHEMU YA BAJETI HII
Usiikose hii. Tusikilize upate fursa, ubadili maisha yako kiuchumi. Tenda Radio imekita kambi jijini Arusha, kuzichambua fursa ya bajeti ya zaidi ya Sh. 104 Bilioni zilizowekwa kwenye Mfumo wa NeST na Halmashauri ya Jiji la Arusha, na jinsi wewe unavyoweza kupata sehemu ya bajeti hiyo. Tuko na Mkurugenzi wa Jiji hilo, Mhandisi Juma Hamsini na walioshinda tenda wanafunguka siri ya ushindi. Tufuate Instagram: @tendaradiotz @ppra_tanzania
-
2
HATUA TATU MUHIMU KUPATA TENDA ZA SERIKALI
Hii ni sehemu ya pili ya Tenda Radio inayokupa hatua tatu muhimu za jinsi ya kupata tenda za Serikali. Tumeyajenga na Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa na Meneja wa Huduma za Kanda wa PPRA, Bi. Vicky Mollel.. Walioshinda tenda za Serikali pia kupitia Mfumo wa NeST wametupatia siri ya ushindi wao.
-
1
JINSI YA KUPATA TENDA ZA SERIKALI KUPITIA MFUMO WA NeST
#KIMEPEWA NGUVU NA PPRA #KAMATA FURSAUnawezaje kupata Tenda ya Serikali kwa haki kupitia Mfumo wa NeST? Kipindi hiki kitakufungua kuhusu jinsi ambavyo unaweza kupata tenda za Serikali (zabuni za umma) kupitia Mfumo wa NeST, na kupata sehemu ya bajeti ya zaidi ya Sh. 25 Trilioni zilizowekwa kwenye mfumo huo. Kwenye episode hii utawasikia wazabuni walioshinda zabuni, wakieleza siri ya mafanikio yao, utawasikia wakuu wa vitengo vya ununuzi Serikalini watakaoeleza kiasi cha fedha walichotenga kwa ajili yako mzabuni na jinsi wanavyoandaa zabuni.Pia, utawasikia Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) wakieleza kwa kina kuhusu ufanisi wa Mfumo na michakato ya ununuzi wa umma.
We're indexing this podcast's transcripts for the first time — this can take a minute or two. We'll show results as soon as they're ready.
No matches for "" in this podcast's transcripts.
No topics indexed yet for this podcast.
Loading reviews...
ABOUT THIS SHOW
TENDA RADIO ni ‘podcast radio’ iliyojikita katika kuwafahamisha, kuwaelimisha na kuwahamasisha wasikilizaji kuhusu fursa za tenda za Serikali, na jinsi ya kupata fursa ya kujipatia fedha za ununuzi wa umma kupitia Mfumo wa NeST. Pia, maudhui haya yanaruka kupitia radio washirika wetu nchini Tanzania ikiwemo Radio Free Afrika, C-FM (Dodoma), A FM (Dodoma), Uyui FM (Tabora), Jembe FM (Mwanza) na nyingine. Imepewa nguvu na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).
HOSTED BY
Tenda Radio TZ
Loading similar podcasts...