Watushule Swahili Podcast podcast artwork

PODCAST · education

Watushule Swahili Podcast

Podikasti ya WatushuleTunafikiri, basi tunakuwa.Watushule ni podikasti kwa watu wanaotaka kuishi maisha yenye mwelekeo na uelewa mzuri. Kila kipindi kinazungumzia mambo muhimu yanayoathiri maisha yetu — kama kusudi, nidhamu, utambulisho, kazi, na hali halisi ya maisha ya Mwafrika katika dunia ya leo.Hii si motisha.Hii ni fikra.Kama unahisi kuna zaidi katika maisha kuliko yale uliyozoea au kuambiwa…basi hii ni sehemu sahihi kwako. www.watushule.com

  1. 8

    Usitafute mafanikio. Tafuta njia za kutokufeli

    Kuna vitu vingi sana vinahitajika kutokea kwenye maisha kuketa mafanikio. Na vitu hivi havipo kwenye uwezo wetu muda mwingi. Lakini kuna vitu vingi sana ambavyo vinafelisha watu, hivi vitu ni rahisi kuviona na kuvifanyia kazi. Episode ya leo tunaangalia kwa undani modo ya kufikiria (mental model) ya kuwaza vitu kinyume. Badala ya kuangalia vitu vya kusaidia mafanikio tunaangalia vitu vya kuzuia kufeli. This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit www.watushule.com

  2. 7

    Malengo yanakusaidia kuanza. Mifumo inakusaidia kumaliza.

    Wengi wanaishi na ndoto ambazo hazina malengo. Wenye malengo hawana sababu yenye nguvu zaidi kuwafanya wavumilie mambo yakiwa magumu. Wenye sababu hawana mfumo mzuri wa kutimiza malengo hayo. Episode hii inaangalia namna bora ya kutengeneza malengo na mifumo ili kutimiza ndoto na matamanio yetu duniani. This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit www.watushule.com

  3. 6

    Kuna tofauti kati yako na kazi yako

    Katika episode hii ya Watushule, ninatafakari maana ya kazi kupitia hatua mbalimbali za maisha.Kutoka kazi za shambani utotoni, kuuza matunda na mboga kwa ajili ya pesa ya matumizi, hadi maisha ya kazi katika mazingira ya kitaaluma na safari ya kujenga miradi mbalimbali huku nikirudi tena na tena kwenye upendo wa usimulizi wa hadithi, episode hii inaangalia ukweli mmoja muhimu:Kuna tofauti kati yako na kazi yako.Binadamu hufanya kazi kwa sababu tofauti katika nyakati tofauti za maisha. Wakati mwingine tunafanya kazi ili kuishi. Wakati mwingine tunafanya kazi kwa pesa. Wakati mwingine tunafanya kazi kwa ajili ya kukua. Na wakati mwingine tunafanya kazi kwa sababu tunaipenda.Lakini matatizo huanza pale kazi inapogeuka kuwa utambulisho.Unapoanza kufikiri kuwa cheo chako ndiyo thamani yako, biashara yako ndiyo wewe mwenyewe, au matokeo yako ndiyo kipimo cha utu wako, kazi inaanza kubeba mzigo ambao haikupaswa kubeba.Episode hii inaangazia historia ya kazi, mvutano kati ya pesa, kufanya unachopenda, na ukuaji, pamoja na hekima ya kujua ni kitu gani kinapaswa kuongoza katika kila msimu wa maisha.Kwa sababu kazi ni sehemu ya maisha.Lakini siyo jumla ya wewe ulivyo.Fikiri kwa kina. Ishi kwa makusudi. This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit www.watushule.com

  4. 5

    Kutokuwa na ugonjwa haimaanishi una afya

    Nini maana halisi ya kuwa na afya?Katika kipindi hiki cha Watushule, natafakari maisha ya bibi yangu Anna, ambaye aliendelea kuwa mwenye nguvu, mwenye bidii, na mwenye utulivu wa ndani hata hadi uzee. Katika siku yake ya kuzaliwa ya miaka 100, nilipomuuliza siri ya afya yake, alitabasamu na kusema, “Mimi ni binti mpendwa wa Mungu.”Miaka mingi baadaye, baada ya kifo chake, jibu hilo lilianza kuwa na maana kubwa zaidi.Kipindi hiki kinachunguza nguzo tatu za afya: mwili, akili, na roho. Kinaangalia kuupa mwili mazoezi, lishe, na mapumziko; uwazi, nidhamu, na amani; maana ya maisha, kuishi kwa kulingana na maana hiyo, na kuishi kwa ajili ya kitu kikubwa kuliko wewe mwenyewe.Kwa sababu afya ya kweli si tu kutokuwepo kwa ugonjwa.Ni ukamilifu wa maisha.Mwili wako hubeba uhai.Akili yako hutafsiri uhai huo.Roho yako huupa uhai huo maana.Fikiri kwa kina. Ishi kwa makusudi. This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit www.watushule.com

  5. 4

    Mahusiano ni muhimu sana kwenye maisha, na bado ndio chanzo cha maumivu makubwa sana kwa watu.

    Mahusiano ni muhimu zaidi kwenye maisha, na ndio yenye changamoto zaidi maishani.Kwenye episode hii ya Watushule Podcast tunaangalia misingi mikuu ya mahusiano: Familia, marafiki na mapenzi.Kwa kuangalia historia za familia, filosofi na mifano hai, episode hii inaangalia namna gani familia inaweza kukujenga au kukharibia msingi wa maisha yako. Tunaangalia namna wewe ni wastani wa marafiki zako watano. Tunaangalia misingi mikuu ya kupunguza maumivu na changamoto kwenye mahusiano ya kimapenzi.Episode hii ni mihimu kwasababu inaangalia kwanini binadamu hawezi kuishi bila watu wengine, na kwanini watu hao hao ndio chanzo kikubwa cha maumivu.Lengo sio kuwa na mahusiano yaliyokamilika.Lengo ni kuwa na mahusiano bora kwa ajili yakoWatushuleFikiria kwa kina. Ishi kwa makusudi. This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit www.watushule.com

  6. 3

    Mambo Muhimu Maishani Huja kwa Utatu, Lakini Maisha Huja Mara Moja Tu

    Kipindi cha 2: Mambo Muhimu Maishani Huja kwa Utatu, Lakini Maisha Huja Mara Moja TuKatika kipindi hiki cha Watushule, tunaacha Kidogo Kungwi’s kwa undani zaidi katika nguzo tatu za maisha — mahusiano, kazi, na afya — ili kuukabili ukweli unaozipa mambo hayo uharaka na muhimu wake: KIFO kwa mwanadamu.Maisha hubadilika kwa misimu. Katika hatua tofauti za maisha, mambo tofauti huwa na uzito tofauti. Lakini nyuma ya yote hayo kuna ukweli mmoja ambao mara nyingi tunaukwepa: muda wetu ni mfupi.Kipindi hiki tutatazama kifo si kama jambo la kuogopa, bali kama mmoja wa walimu wakubwa wa maisha. Kupitia falsafa, maumivu binafsi ya kupoteza, na tafakari ya kweli, Watushule inachunguza jinsi kukumbuka kifo kunavyoweza kutusaidia kuishi kwa ujasiri zaidi, nidhamu zaidi, shukrani zaidi, na kusudi zaidi.Kama maisha huja mara moja tu, tunapaswa kuyaishije?Fikiri kwa kina. Ishi kwa makusudi. This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit www.watushule.com

  7. 2

    Vitu vya muhimu kwenye maisha vinaonekana kuja kwa tatu

    This is a public episode. If you would like to discuss this with other subscribers or get access to bonus episodes, visit www.watushule.com

Type above to search every episode's transcript for a word or phrase. Matches are scoped to this podcast.

Searching…

We're indexing this podcast's transcripts for the first time — this can take a minute or two. We'll show results as soon as they're ready.

No matches for "" in this podcast's transcripts.

Showing of matches

No topics indexed yet for this podcast.

Loading reviews...

ABOUT THIS SHOW

Podikasti ya WatushuleTunafikiri, basi tunakuwa.Watushule ni podikasti kwa watu wanaotaka kuishi maisha yenye mwelekeo na uelewa mzuri. Kila kipindi kinazungumzia mambo muhimu yanayoathiri maisha yetu — kama kusudi, nidhamu, utambulisho, kazi, na hali halisi ya maisha ya Mwafrika katika dunia ya leo.Hii si motisha.Hii ni fikra.Kama unahisi kuna zaidi katika maisha kuliko yale uliyozoea au kuambiwa…basi hii ni sehemu sahihi kwako. www.watushule.com

HOSTED BY

Waafrika wanaofikiria.

CATEGORIES

Frequently Asked Questions

How many episodes does Watushule Swahili Podcast have?

Watushule Swahili Podcast currently has 7 episodes available on PodParley. New episodes are automatically indexed when they're published to the podcast feed.

What is Watushule Swahili Podcast about?

Podikasti ya WatushuleTunafikiri, basi tunakuwa.Watushule ni podikasti kwa watu wanaotaka kuishi maisha yenye mwelekeo na uelewa mzuri. Kila kipindi kinazungumzia mambo muhimu yanayoathiri maisha yetu — kama kusudi, nidhamu, utambulisho, kazi, na hali halisi ya maisha ya Mwafrika katika dunia ya...

How often does Watushule Swahili Podcast release new episodes?

Watushule Swahili Podcast has 7 episodes. Check the episode list to see recent publication dates and frequency.

Where can I listen to Watushule Swahili Podcast?

You can listen to Watushule Swahili Podcast on PodParley by clicking any episode. We provide an embedded audio player for direct listening, and you can also subscribe via your preferred podcast app using the RSS feed.

Who hosts Watushule Swahili Podcast?

Watushule Swahili Podcast is created and hosted by Waafrika wanaofikiria..
URL copied to clipboard!