PODCAST · business
Ongea na Coach Makirita Amani's show
by Dr Makirita Amani
Ongea na Coach Makirita Amani ni mafunzo kwa njia ya sauti yanayotolewa na Kocha Makirita Amani, ambaye ni mwandishi, mjasiriamali na kocha wa mafanikio.Sikiliza vipindi hivi kujifunza na kuchukua hatua ili uweze kufanikiwa.Pia tembelea www.amkamtanzania.com na www.kisimachamaarifa.co.tz ili kujifunza zaidi.Karibu sana.
-
9
#DZK020; Hamasa, Jasho Na Hatari Kwenye Safari Ya Mafanikio Makubwa.
Hamasa, Jasho na Hatari Rafiki, Mafanikio makubwa yanaenda kwa kanuni hii; 1. Hamasa - 10% 2. Jasho (Kazi) - 90% 3. Hatari - Mara zote. Watu wengi wanakwama kufanikiwa kwa sababu wanageuza kanuni hiyo. Wanadhani hamasa pekee inawatosha kufanikiwa. Wanakwepa kuweka kazi kubwa inayohitajika. Na wanakwepa hatari. Kama unafanya chochote kati ya hivyo, jua unajikwamisha mwenyewe kufanikiwa. Kwenye #BaruaYaKocha nimekueleza kwa kina hayo matatu na jinsi ya kuyatumia kujenga mafanikio makubwa. Isome barua hiyo hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Mafanikio yako yanategemea sana mambo ya ndani yako kuliko ya nje. Weka vizuri ndani ufanikiwe.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
8
#DZK019; Tumaini Unalohitaji Ili Kufanikiwa Kwa Uhakika
Ukiwa na Tumaini Hili, Hakuna Kitakachokushinda. Rafiki, Pamoja na wengi kutaka mafanikio makubwa kwenye maisha yao, Ni wachache sana wanaoyapata. Na siyo kwa sababu mafanikio yamewekwa kwa ajili ya wachache. Bali ni kwa sababu wengi wanakosa Tumaini la kuendelea na safari, hasa mambo yanapokuwa magumu. Kwenye #BaruaYaKocha nimekushirikisha Tumaini ambalo ukilijenga, hakipo kinachoweza kukuangusha. Hii ni barua inayokufungua na kuondoa kila kizingiti kilicho ndani yako. Isome barua hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Tumaini ni kitu muhimu sana kwenye safari ya mafanikio. Hakikisha unayajenga kwa usahihi.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
7
#DZK018; Okoa Muda Na Nguvu, Ufanikiwe.
Unapoteza Rasilimali Muhimu Bila Tija. Rafiki, Muda wako na nguvu zako ni rasilimali muhimu sana kwako. Hizo ndiyo rasilimali kuu zinazohitajika kwenye kujenga mafanikio makubwa. Lakini pia ni rasilimali zenye uhaba mkubwa. Una ukomo wa muda na nguvu zako zinaisha kila unapozitumia. Cha kushangaza, licha ya ukomo wa rasilimali hizo, umekuwa unazipoteza bila tija. Umekuwa unafanya mambo yanayotumia vibaya rasilimali hizo muhimu. Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha mambo matano unayopenda sana kuyafanya yanayopoteza rasilimali hizo. Hakikisha unayajua na kuacha kuyafanya ili usijikwamishe kufanikiwa. Soma barua hiyo hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Tumia vizuri rasilimali ulizonazo ili uweze kufanya makubwa.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
6
#DZK017; Raha Rahisi Zinakupoteza
RAHA RAHISI, MAFANIKIO MAGUMU. Rafiki, Moja ya vitu vinavyokuzuia kupata mafanikio makubwa ni raha unazopata kwa urahisi. Mambo mengi tunayofanya ni kwa ajili ya kupata raha. Na pale raha inapopatikana kirahisi, kama kupitia ulevi, mitandao na kufanya mapenzi, inazuia kufanya makubwa yanayohitajika kwenye mafanikio. Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha jinsi ya kukwepa mtego huo wa Raha Rahisi ili uweze kupata mafanikio makubwa. Karibu usome barua hiyo hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Usipokuwa makini, utahangaika na mengi na usifanikiwe.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
5
#DZK016; Jiamini Kupitiliza Upate Mafanikio Makubwa
MAFANIKIO MAKUBWA HAYATOKANI NA AKILI ZA KAWAIDA. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Umekuwa unayataka mafanikio makubwa, Lakini hujayapata mpaka sasa. Siyo kwa sababu haiwezekani, Bali kwa sababu njia unazotumia siyo sahihi. Njia kuu inayokupotosha ni wewe kutumia akili zako za kawaida. Hizo ndiyo akili zimekufikisha hapo ulipo sasa. Na kamwe, haziwezi kukufikisha zaidi ya hapo ulipo. Kupata matokeo ya tofauti, lazima ufanye mambo ya tofauti. Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha aina ya akili za tofauti unazohitaji ili ujenga mafanikio makubwa. Isome barua hiyo hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, unaweza kabisa kujenga mafanikio makubwa. Ila cha kwanza, acha kutumia akili zako za kawaida.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
4
#DZK015; Fanikiwa Bila Kutegemea 'Koneksheni'
Uhakika Wa Mafanikio Kama Unaanzia Chini. Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki yangu mpendwa, Unaanzia chini kabisa, Huna koneksheni, Huna akili nyingi, Huna urithi, Na huna fursa ambazo wengine wanazipata. Je kuna nafasi yoyote kwako kufanikiwa? Jibu ni NDIYO KUBWA. Mafanikio makubwa hayategemei sana unaanzia wapi, Bali yanategemea unaelekea wapi. Kwenye #BaruaYaKocha nimekueleza mambo ya kusimamia ili ufanikiwe, hata kama unaanzia chini kabisa. Mambo hayo tayari yapo ndani yako, ni wewe tu uchague kuyafanyia kazi na upate matokeo. Isome barua hiyo hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Usilalamikie tena uliyokosa, bali tumia vizuri hayo uliyonayo sasa ufanikiwe.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
3
#DZK014; Unajinyima Pesa Wewe Mwenyewe.
#BZK; KWA NINI UNAUPENDA SANA UMASIKINI? Soma hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, Huenda hilo swali limekushtua, Kwa sababu umekuwa unadhani kwamba unauchukia umasikini. Kwamba unapambana usiku na mchana ili uondoke kwenye umasikini. Lakini tunapoangalia mambo unayofanya, tunaona kabisa ni kinyume na hilo. Na hata matokeo unayopata sasa, yanaakisi kabisa hilo. Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha mambo unayofanya sasa, ambayo yanakukwamisha kupata pesa. Na hata unapozipata, hazikai, bali unapoteza zote. Ni mambo unayoona ya kawaida, lakini ni kikwazo kikubwa kwako. Isome barua hiyo ili uache kujikwamisha. Fungua hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Rafiki, unakazana sana lakini unajikuta umebaki hapo hapo. Kuna maeneo unajihujumu, yajue na uache kujikwamisha.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
2
#BZK013; Jinsi ya Kujenga Biashara Kubwa Hata Kama Huna Mtaji.
Biashara Bila Mtaji? Rafiki, Najua upo kwenye moja ya makundi haya mawili; Moja; Hujaanza biashara kwa sababu huna mtaji. Mbili; Una biashara ila haikui, kwa sababu huna mtaji. Ninachotaka kukuambia ni hiki; hakuna kundi sahihi hapo wewe kuwa. Unaweza kuanzisha na kukuza biashara kwa mafanikio makubwa, hata kama huna mtaji. Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha jinsi ya kufanya hivyo kwa uhakika. Isome barua hiyo hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Usisingizie tena mtaji, tumia vizuri rasilimali ulizonazo.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
1
#DZK012; Mfurahishe Mtu Huyu Mmoja Pekee Ili Ufanikiwe.
Unajiangusha sana wewe mwenyewe. Rafiki, Kila unachofanya kwenye maisha yako, una bet kwenye furaha. Unadhani utakuwa na furaha zaidi kwa kufanya kitu hicho kuliko kutokukifanya. Mara nyingi, unashindwa kwenye kubet kwako, kwa sababu unaweka dau lako pasipo sahihi. Unaweka dau lako kwenye kutaka kuwafurahisha wengine. Wakati hilo ni jukumu usiloliweza kabisa. Una jukumu moja tu hapa duniani, kujifurahisha wewe mwenyewe. Ukilitimiza hilo, utapata kila unachotaka. Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha jinsi ya kujipa furaha bila ya kujiona mwenye hatia. Nimekuweka huru uyafurahie maisha yako, hata kama bado hayajakamilika. Karibu uisome barua hiyo hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Jibetie wewe mwenyewe kwenye furaha yako, Na mkeka wako wa mafanikio utatiki.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
0
#DZK011; Usivurugwe Na Mapenzi Kwenye Safari Ya Mafanikio.
Makosa Ya Kufanya Unachopenda. Rafiki, Ushauri wa mtu kufanya kile anachopenda ndiyo afanikiwe umewapoteza wengi sana. Kwenye mengi ambayo watu wanapenda kufanya, hayawezi kuwapa mafanikio wanayotaka. Swali ni je wewe unachukua hatua gani pale unachopenda kufanya hakiwezi kukupa mafanikio? Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha jinsi ya kutokuvurugwa na kufanya unachopenda kwenye safari ya mafanikio. Isome Barua hiyo hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Usikubali kuvurugwa na mapenzi kwenye safari ya mafanikio.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-1
#DZK010; Vigezo Viwili Vya Kuamua Cha Kufanya Ili Ufanikiwe.
Kama Unachofanya Kinakidhi Vigezo Hivi 2, Wapuuze Wanaokupinga. Rafiki, Safari ya mafanikio ina vikwazo na changamoto nyingi. Kuna miluzi mingi sana, ambapo kama hutakuwa makini, itakupoteza. Ili usipotezwe na hiyo miluzi mingi, kuna vigezo vikuu viwili unavyotakiwa kutumia kuchagua nini ufanye na nini upuuze. Kwenye #BaruaYaKocha nimeeleza kwa kina vigezo hivyo na jinsi ya kuvitumia. Isome barua hiyo hapa; Usiyumbishwe tena, jifunze kufanya maamuzi sahihu kwako.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-2
#DZK009; Chagua Kwa Usahihi Kitakachokuua.
KUBALI MAFANIKIO MAKUBWA YAKUUE. Rafiki, Kabla hujashtushwa na hilo, Nikukumbushe tu kwamba, *utakufa*. Na hutakufa tu hivi hivi, bali kuna kitu kitakachokuua. Swali ni je unachagua nini kikuue? Utakuwa tayari kukwepa kufanya kazi ngumu inayohitajika ili ufanikiwe, Halafu ufe kwa ulevi au ajali za kizembe? Unapoyakimbia mafanikio kwa sababu yana hatari, Unakuwa umezikubali hatari nyingine na kuiacha ya mafanikio. Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha jinsi unavyoweza kuchagua kwa usahihi kitakachokuu na hilo kukupa mafanikio makubwa sana. Isome barua hiyo hapa; https://learn.tanzaniteskills....Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-3
#DZK008; Mafanikio Ni Kujua Hujui.
MAFANIKIO NI KUJUA HUJUI. Rafiki, Unapoianza safari ya mafanikio, unakuwa hujui na hivyo unajifunza. Unapoanza kupata mafanikio, unaanza kuona tayari unajua na hivyo hujifunzi tena. Hapo ndipo unapokaribisha anguko la kimafanikio. Ili kupata na kudumu kwenye mafanikio makubwa, unapaswa kujua kitu kimoja; *JUA KWAMBA HUJUI* Kwa kujua hujui, unakuwa mnyenyekevu na kujifunza bila kukoma. Kwenye #BaruaYaKocha nimekushirikisha mambo matano ya kukuweka kwenye kujifunza endelevu ili kujenga mafanikio makubwa. Isome barua hiyo hapa; https://learn.tanzaniteskills....Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-4
#DZK007; Usikubali Kushindwa Na Yeyote
USIKUBALI KUSHINDWA NA YEYOTE. Rafiki, Ushindani ni sehemu ya safari yako ya mafanikio. Lolote utakalofanya na kuleta matokeo mazuri, watu watakuiga. Huwezi kuwashinda wengine kwa kushindana nao moja kwa moja. Badala yake kuna mbinu bora kabisa za kuwashinda wengine bila kusumbuka sana. Kwenye #BaruaYaKocha, nimekuonyesha mambo matano ya kukuwezesha kuwashinda wengine wote. Yajue mambo hayo kwa kusoma hapa; https://learn.tanzaniteskills....Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-5
#DZK006; Pesa Inaweza Kununua Furaha.
PESA INAWEZA KUNUNUA FURAHA Rafiki, Najua umeaminishwa kwamba utajiri hauwezi kukupa furaha. Na hiyo ndiyo sababu unakosa vyote, unakosa utajiri na pia unakosa furaha. Ili uweze kupata vyote, upate utajiri mkubwa na uwe na furaha, kuna mambo matano muhimu kuzingatia. Kwenye #BaruaYaKocha nimekushirikisha mambo hayo na jinsi ya kuyatumia kujenga utajiri na furaha. Soma barua hiyo hapa; https://learn.tanzaniteskills.... Pesa zinanunua furaha vizuri kabisa, kama unajua inakouzwa. Soma Barua ya Kocha, ujue hilo kwa uhakika.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-6
#DZK005; Baki Na Njaa Kali Ya Mafanikio Milele
BAKI NA NJAA KALI YA MAFANIKIO. Rafiki, Unapokuwa unaanzia chini, unakuwa na njaa kali ya mafanikio. Njaa hiyo inakusukuma kufanya mambo makubwa na kupata matokeo makubwa. Lakini unapoanza kupata matokeo mazuri, hiyo njaa inaondoka. Na hapo ndipo anguko la wengi linapoanzia. Kama unataka kupata na kudumu kwenye mafanikio makubwa, unatakiwa kubaki na njaa kali ya mafanikio uliyoanza nayo. Kwenye #BaruaYaKocha nimekushirikisha jinsi ya kufanya hivyo. Isome barua hapa; https://learn.tanzaniteskills....Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-7
#DZK004; Endelea Na Safari Ya Mafanikio Hata Mambo Yanapokuwa Magumu.
ENDELEA HATA KAMA MAMBO NI MAGUMU Rafiki, Safari ya mafanikio makubwa haijawahi kuwa rahisi. Unaweza kujua unachotaka na ukaweka juhudi kubwa. Lakini bado matokeo yakawa tofauti na matarajio. Hapo ndipo wengi hukata tamaa na kuacha. Kwenye #BaruaYaKocha nimekupa sababu 5 za kwa nini unapaswa kuendelea hata mambo yanapokuwa magumu. Isome barua hiyo hapa; https://learn.tanzaniteskills....Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-8
#DZK003; Furahia Kutokueleweka Na Wengine
Furahia Kutokueleweka Na Wengine. Rafiki, Utakapofanya zoezi la *KWA NINI SABA* na ukalijua kusudi la maisha yako na ndoto zako kubwa, Utagundua kwamba uko tofauti kabisa na kila mtu. Watu wote wanaokuzunguka hawatakuelewa. Watakuona kama mtu uliyechanganyikiwa na utakayeenda kushindwa. Wengi wanakwamishwa na hilo na kushindwa kufanikiwa. Kama wewe unataka kufanikiwa, *lazima ufurahie kutokueleweka na wengine.* Kwenye #BaruaYaKocha nimeeleza jinsi ya kutekeleza hilo. Isome barua hapa; https://learn.tanzaniteskills....Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-9
#DZK002; Kwa Nini Saba Zitakazokupa Mafanikio Makubwa.
KWA NINI 7 ZITAKAZOKUPA MAFANIKIO MAKUBWA Rafiki yangu mpendwa, Ulikuja hapa duniani bila maelekezo yoyote ya unachoweza kufanya na kwa nini uko hapa duniani. Siyo kwa sababu umekuja hapa duniani bahati mbaya, bali kwa sababu majibu yako ndani yako. Lakini kwa bahati mbaya sana, hujawahi kupata nafasi ya kujua majibu hayo. Kwenye #BaruaYaKocha nimekupa mchakato wa KANUNI 7 utakaokuwezesha kujua KUSUDI LA MAISHA YAKO. Kwenye #Dakika10ZaKocha nimefafanua pia kuhusu mchakato huo. Hiki ni kitu unachopaswa kukielewa kama kweli umedhamiria kupata mafanikio makubwa. Soma barua hapa; https://learn.tanzaniteskills....Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-10
#DZK001; Rudia Rudia Bila Kuchoka (MAKIRITA 10 X 10 KILA SIKU)
Rudia Rudia Bila Kuchoka Rafiki, Kwa kipindi ambacho nimejifunza na kuishi kanuni za mafanikio, Kuna kitu kimoja nimeona kinawatenganisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa. Kitu hicho ni uwezo wa kurudia rudia mambo yanayochosha bila kuchoka. Kwenye #BaruaYaKocha nimekushirikisha mambo 10 (MAKIRITA 10 × 10 KILA SIKU) ninayoazimia kuyafanya kwa kurudia rudia kila siku bila kuacha. Karibu ujifunze mambo hayo, ili na wewe uweze kupanga utakayofanya. Na kama utataka tushirikiane kwa karibu katika kuyaishi, nafasi hiyo ipo. Isome barua hapa, https://learn.tanzaniteskills.... Pia sikiliza #Dakika10ZaKocha ambapo nimefafanua hilo.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-11
#DZK000; Kwa Heri Mashine, Karibu Tena Binadamu.
Kwa Heri Mashine, Karibu Tena Binadamu. Rafiki, Ujio wa Akili Mnemba (AI) umeleta mapinduzi na manufaa makubwa. Lakini pia umekuja na hatari ya kupoteza kitu pekee ambacho kimekuwa kinatutofautisha sisi binadamu na viumbe wengine. Kwenye #BaruaYaKocha nimekuonyesha hilo na jinsi ya kuliepuka. Pia kwenye #Dakika10ZaKocha, nimefanua kwa kina. Soma barua hapa; https://learn.tanzaniteskills....Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-12
#DZK009; Hakuna Mbadala Wa Ubora Wa Juu Kwenye Mafanikio Makubwa
🔥 UTAJIRI, HESHIMA NA FURSA HAVIENDI KWA WATU WA KAWAIDA. Dunia inakulipa kwa kiwango cha UBORA unaouonyesha kila siku. Kila jambo lina maana. Kila tabia ina gharama. Kila uzembe unakupunguzia thamani. ⚠️ Watu wengi wanataka maisha makubwa huku wakifanya vitu kwa kiwango cha chini. Na hapo ndipo wanapopoteza kila kitu bila kujua. #BaruaYaKocha itakufundisha kwa nini: ✅ Ubora ni mfumo wa maisha ✅ Dunia inakuhukumu kwa sehemu yako mbaya zaidi ✅ Mambo madogo ndiyo yanayojenga mafanikio makubwa ✅ Watu wa kiwango cha juu hawaishi kwa mazoea 💥 Kama unataka kuingia kwenye asilimia 10 ya watu wanaofanya vizuri sana, usikose kusoma barua hii. Fungua hapa; https://learn.tanzaniteskills....Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-13
#DZK008; Fanya Kwa Kupitiliza
🔥 Watu wengi wanabaki wa kawaida kwa sababu wanaogopa kuonekana “wamepitiliza.” Ukitaka fedha kubwa, mafanikio makubwa, na maisha makubwa… lazima ukubali: ✔️ Kusemwa ✔️ Kuonekana tofauti ✔️ Kufanya kazi kupita kawaida ✔️ Kuwa na moto ambao watu wengine hawauelewi Usipunguze makali yako ili kuwafanya watu wengine wajisikie vizuri. 🚀 #BaruaYaKocha itabadilisha namna unavyoona mafanikio, kazi, na maoni ya watu kuhusu maisha yako. 🔥 Fungua hapa; https://learn.tanzaniteskills....Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-14
#DZK007; Usipojipanga, Utapangwa.
🔥 WATU WENGI HAWAISHI MAISHA YAO… WANATEKELEZA MAAGIZO YA JAMII. Ukikosa kuchagua maisha yako, dunia itakuchagulia. Ukikosa kusudi lako, utaishi kwa kuwafurahisha wengine. Ukikosa mfumo wako, utaendeshwa na mfumo wa watu wengine. #BaruaYaKocha itakufungua macho kuhusu: ✔️ Kwa nini watu wengi hupoteza mwelekeo wa maisha ✔️ Jinsi jamii inavyokuibia ndoto zako taratibu ✔️ Kwa nini kufuata kundi ni hatari kubwa ✔️ Namna ya kujenga maisha yako mwenyewe kwa ujasiri mkubwa Kama unahisi maisha yako yanaendeshwa na mazingira kuliko maamuzi yako mwenyewe, hii barua ni kwa ajili yako. Soma mpaka mwisho. Inaweza kubadilisha kabisa namna unavyoishi maisha yako. 🔥 Fungua hapa; https://learn.tanzaniteskills....Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-15
#DZK006; Swali Pekee Litakalokukomboa Kimafanikio
🚨 UCHOVU WAKO HAUTOKANI NA KAZI NYINGI… BALI VITU VISIVYO NA MAANA! 🚨 Watu wengi wako bize… Lakini maisha yao hayasogei mbele. 😔 📌 Maneno mengi yasiyo na faida. 📌 Mijadala isiyo na matokeo. 📌 Simu na mitandao inayomeza muda. 📌 Watu wanaonyonya nguvu na umakini wako. Kwenye #BaruaYaKocha utajifunza: 🔥 Kwa nini maisha yako yamejaa kelele zisizo muhimu 🔥 Jinsi ya kupata utulivu, muda na umakini mkubwa 🔥 Sababu watu wenye mafanikio hujifunza kusema HAPANA 🔥 Swali moja rahisi linaloweza kubadilisha maisha yako kabisa ⚠️ Ukimaliza kusoma barua hii, hutatazama muda wako kwa namna ileile tena. SOMA SASA. 🧠🔥 Fungua hapa; https://learn.tanzaniteskills....Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-16
#DZK005; Jua Hasa Unachotaka, Uwe Hatari Kwenye Mafanikio
⚠️🧠 UKIJUA HASA UNACHOTAKA, UNAKUWA MTU HATARI SANA KWENYE MAFANIKIO Watu wengi wanaishi maisha ya kuchoka, kuhangaika na kuzunguka sehemu moja, Kwa sababu hawajajua hasa wanataka nini. Nguvu zao zinatawanyika kila upande. 😓 Lakini siku utakapojua hasa unachotaka kwenye maisha yako… Unakuwa MTU HATARI sana kwenye mafanikio. 🔥💣 Unaanza kuona usumbufu kama adui. ⛔ Unaanza kutumia muda kwa makusudi. ⏳ Unaanza kufanya maamuzi makubwa bila kuogopa. 🎯 Na maisha yako yanaanza kwenda mbele kwa kasi ambayo watu hawaielewi. 🚀 #BaruaYaKocha itakufungua macho kuhusu nguvu kubwa ya kuwa na mwelekeo mmoja wa maisha. Soma kwa makini sana. 👇🔥 Fungua hapa; https://learn.tanzaniteskills....Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-17
#DZK004; Akili Tulivu Ndiyo Silaha Ya Mafanikio Makubwa
😰🧠 JE, MATATIZO YANAKUNYIMA USINGIZI? Watu wengi hawashindwi kwa sababu hawana uwezo. Wanashindwa kwa sababu akili zao zimejaa mawazo, hofu, na wasiwasi usioisha. Usiku wanashindwa kulala. Asubuhi wanaamka wamechoka. Na siku nzima wanapambana wakiwa tayari wameishiwa nguvu. Lakini kuna siri kubwa ya watu waliofanikiwa sana duniani: 🧠 Wanajifunza "kufuta ubao wa akili zao." 😴 Wanalala kwa nguvu sawa na wanavyofanya kazi kwa nguvu. 💪 Hawaruhusu matatizo yawaelemee. 🎯 Wanashughulikia tatizo moja kwa wakati mmoja. Katika #BaruaYaKocha ya leo utajifunza: ✅ Jinsi ya kuzuia matatizo yasikuvunje kiakili ✅ Mbinu rahisi ya kutuliza akili kabla ya kulala ✅ Siri ya kupata nguvu mpya kila siku ✅ Namna ya kufanya kazi kwa kiwango cha juu kwa miaka mingi Ukijifunza kuitawala akili yako, hakuna tatizo litakaloweza kuitawala ndoto yako. 🔥 Soma barua hii sasa. Inaweza kubadilisha jinsi unavyokabiliana na changamoto zako kuanzia leo. Fungua hapa; https://learn.tanzaniteskills....Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-18
#DZK003; Endea Ndoto Zako Kwa Ujasiri Mkubwa
🚀 NDOTO ZAKO HAZITATIMIA KWA KUZITAMANI TU. Mwandishi Henry David Thoreau aliandika: “Ukisonga kwa ujasiri kuelekea ndoto zako, na kuamua kuishi maisha unayoyawazia, utakutana na mafanikio ambayo watu wengi hawakuyatarajia.” 🔥 Hii ndiyo siri ya mafanikio makubwa. Watu wengi wana ndoto. Wachache wanaanza. Na wachache zaidi wanaendelea mpaka washinde. 💡 Ukisubiri mpaka ujisikie tayari, unaweza kusubiri maisha yako yote. 💡 Ukianza leo, dunia inaweza kukufungulia milango usiyowahi kuifikiria. 💡 Mafanikio huwapenda watu wenye ujasiri wa kuchukua hatua. 📈 Ndoto kubwa. 💪 Ujasiri mkubwa. 🚶 Hatua za kila siku. 🏆 Mafanikio makubwa. Usikubali ndoto zako zife ndani yako. Soma #BaruaYaKocha ujifunze jinsi ya kusonga kwa ujasiri kuelekea maisha uliyokusudiwa kuishi. Fungua hapa; https://learn.tanzaniteskills....Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-19
#DZK002; Salama Ni Hatari Zaidi Kwa Mafanikio Yako.
🔥💰 NJIA INAYOONEKANA SALAMA NDIYO HATARI KUBWA ZAIDI! ⚠️🚀 Watu wengi wanaogopa kuacha ajira, kuanza biashara, kuhama kwenda sehemu mpya, au kujitoa kikamilifu kwenye ndoto zao kwa sababu wanaona ni hatari kubwa. 😨 Lakini ukweli ni huu: 🚫 Kutochukua hatua ndiyo hatari kubwa zaidi. 🚫 Kubaki ulivyo ndiyo hatari kubwa zaidi. 🚫 Kuchelewesha ndoto zako ndiyo hatari kubwa zaidi. 🚫 Kuchagua salama ndiyo hatari kubwa zaidi. 💎 Wakati wengine wanaona hatari, wewe unatakiwa kuona fursa. 📖 Kwenye #BaruaYaKocha, utajifunza kwa nini hatua unayoogopa leo inaweza kuwa ndiyo daraja la utajiri mkubwa kesho. 🔥 Kwa mtu mwenye ndoto kubwa, salama ndiyo hatari kubwa zaidi. Fungua hapa; https://learn.tanzaniteskills....Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-20
#DZK001- Neno Kuu La Ushindi - VIZURI
🔥 MAMBO YANAPOHARIBIKA, USISEME “KWA NINI MIMI?” — SEMA NENO MOJA TU: VIZURI. Umekataliwa? VIZURI. Umepoteza fedha? VIZURI. Biashara imeshuka? VIZURI. Mpango umefeli? VIZURI. Changamoto zimeongezeka? VIZURI. Ndani ya kila tatizo kuna somo. Ndani ya kila hasara kuna fursa. Ndani ya kila maumivu kuna nguvu mpya ya kukufanya uwe bora zaidi. Kama bado unapumua, bado unaweza kupigana. Kama bado unaweza kupigana, bado unaweza kushinda. Soma #BaruaYaKocha ujifunze kwa nini washindi wa kweli huona mema hata katikati ya matatizo makubwa. 💪 VIZURI. 🚀 INUKA. 🧠 REKEBISHA. 🔥 SHAMBULIA TENA. 🏆 USHINDI BADO UNAWEZEKANA. Fungua hapa; https://learn.tanzaniteskills....Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-21
JINSI YA KUEPUKA KUTAPELIWA NA FURSA MPYA.
Kila siku kuna fursa mpya zinazoibuka, baadhi ya fursa hizo ni za kweli na nyingi ni za uongo na utapeli. Watu wengi wameumizwa na fursa walizokimbilia wakifikiri wamepata, wakaishia kuwanufaisha wengine. Kwenye kipindi cha leo nakwenda kukushirikisha namna ya kuepuka kutapeliwa na fursa mpga. Jifunze upate maarifa sahihi na uweze kufanya maamuzi sahihi.
-
-22
KITU KIKUBWA KUHUSU MAFANIKIO TUNACHOWEZA KUJIFUNZA KUTOKA KWA WANAJESHI
Kuna kitu kimoja kikubwa tunaweza kujifunza kutoka kwa wanajeshi kuhusu mafanikio. Kitu hicho haijalishi unaanzia wapi au una elimu kiasi gani. Sikiliza kipindi cha leo kujua jinsi ya kutumia kitu hicho ili kufanikiwa.
-
-23
AUDIO; PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU.
Muda umekuwa ni changamoto na kikwazo kwa wengi kufikia malengo yao ya kimaisha. Kila siku tumekuwa tunasema kama ningekuwa na muda wa ziada ninge.... Lakini siku zinakwenda na hatuoni kupatikana kwa muda huo wa ziada. Tunaamua kuzika ndoto zetu kwa sababu hatukupata muda wa kuzifanyia kazi. Vipi leo nikikuambia kwamba unaweza kupata masaa mawili ya ziada kila siku? Ndiyo namaanisha masaa mawili, dakika 120 za ziada kwenye siku yako ya kawaida? Ni mangapi makubwa utaweza kuyafanya na kubadili kwenye maisha yako kwa nyongeza ya masaa mawili kila siku? Kwenye kitabu hiki siyo tu ninakuambia ya kwamba unaweza kupata masaa mawili ya ziada, bali ninakuonesha hatua kwa hatua jinsi unavyoweza kupata hayo masaa mawili ya ziada kila siku kwenye maisha yako. Nitakushirikisha mbinu bora za kuweza kutunza na kutumia vizuri muda wako kila siku, ili uache kusingizia muda kama sababu ya wewe kushindwa kuishi ndoto zako. Baada ya kukuwezesha kuyapata masaa mawili ya ziada kwenye siku yako, sitakuacha nayo halafu uyapoteze, badala yake nitakushauri njia bora za kutumia masaa hayo mawili ya ziada kila siku, uweze kubadili maisha yako na kuwa bora zaidi. Unapokuwa bora basi mafanikio ni uhakika kwako. Karibu twende pamoja kwenye kitabu hiki ili tujifunze njia bora za kutunza na kutumia muda wetu ili kuishi maisha ya mafanikio. Rafiki na Kocha wako, Makirita Amani, [email protected] www.kisimachamaarifa.co.tz www.amkamtanzania.co.tz
-
-24
UNA MUDA WA KUTOSHA
Muda umekuwa changamoto kwa wengi kushindwa kufikia ndoto zao. Wengi wanasema hawana muda, au wakipata muda watafanya kitu fulani. Ukweli ni kwamba huwezi kupata muda, bali unaweza kutenga muda. Sikiliza kipindi cha leo ujifunze namna unavyoweza kutenga muda wa kufanya yale muhimu kwako.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-25
SAA MOJA MUHIMU SANA KWENYE MAISHA YAKO
Katika masaa 24 ya siku, unahitaji kutenga saa moja kwa ajili yako binafsi. Kwa kuweza kuitumia vizuri saa hii moja utaweza kuwa na maisha bora yenye mafanikio makubwa.Sikiliza kipindi hiki ujue njia bora za kuenga na kutumia saa moja kwa ajili yako binafsi.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-26
Hakuna Maisha Kama Hakuna Mabadiliko
Mabadiliko ni kitu ambacho kinapaswa kufanywa kila siku na kila mtu.Kama unataka kuboresha maisha yako, lazima ubadili kitu kila siku.Sikiliza kipindi hiki kujifunza kuhusu mabadiliko.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-27
Fukuza Wateja Hawa.
Siyo kila mtu anaweza kuwa mteja wa biashara yako.Unahitaji kuchagua aina ya wateja ambao utafanya nao biashara na kujua wateja ambao unahitaji kuwaepuka kwenye biashara yako. Sikiliza kipindi hiki cha leo kujua wateja wakuwa nao na wateja wa kuwafukuza.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-28
Usikubali Kirahisi
Kila unachofanya kwenye maisha yako utakutana na changamoto.Je unapambanaje na changamoto hizi?Sikiliza kipindi hiki kupata mbinu za kukabiliana na changamoto unazokutana nazo.Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
-
-29
Kulalamika...
Become a supporter of this podcast: https://www.spreaker.com/podcast/dakika-10-za-kocha--1923276/support.
We're indexing this podcast's transcripts for the first time — this can take a minute or two. We'll show results as soon as they're ready.
No matches for "" in this podcast's transcripts.
No topics indexed yet for this podcast.
Loading reviews...
ABOUT THIS SHOW
Ongea na Coach Makirita Amani ni mafunzo kwa njia ya sauti yanayotolewa na Kocha Makirita Amani, ambaye ni mwandishi, mjasiriamali na kocha wa mafanikio.Sikiliza vipindi hivi kujifunza na kuchukua hatua ili uweze kufanikiwa.Pia tembelea www.amkamtanzania.com na www.kisimachamaarifa.co.tz ili kujifunza zaidi.Karibu sana.
HOSTED BY
Dr Makirita Amani
CATEGORIES
Loading similar podcasts...