PODCAST · news
Wimbi la Siasa
by RFI Kiswahili
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Episodes
-
Chanzo cha kuzuka kwa vita vipya Kaskazini mwa Ethiopia
Tangu tarehe 23 Septemba, mapigano mapya yameendelea kushuhudiwa Kaskazini mwa Ethiopia, kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa Tigray. Nini kinaendelea Ethiopia na vita vina vinaweza kuvuka mipaka ? Mchambuzi wetu ni Abdullahi Boru, mtalaam wa masuala amani , usalama, haki za binadamu…
more -
Suluhu ya njiapanda ya kisiasa nchini Sudan Kusini
Sudan Sudan inakabiliwa na mzozo wa kikatiba na kisiasa, kuelekea uchaguzi mkuu wa kwanza, uliopangwa kufanyika tarehe 22 mwezi Disemba mwaka huu. Rais Salva Kiir, anayetarajiwa kuwania, amebadilisha sheria ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele kuwa uchaguzi huo unatakiwa kufanyika chini ya Katiba...
-
Kenya: Kwanini rais Ruto na mtangulizi wake wanatupiana maneno ?
Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya mwaka 2027, vita vya maneno kati ya rais William Ruto na mtangulizi wake, Uhuru Kenya zimeshika kasi. Nini chanzo cha majibizano haya ? Victor Abuso anachambua hili kwa kina na Edwin Kegoli, mchambuzi wa siasa na masuala ya sera nchini Kenya.
-
Hatima ya serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar
Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi, amezindua Kamati ya pamoja ya majadiliano kati ya chama chake CCM na kile cha upinzani ACT Wazalendo, katika kile kinachoashiria hatua mpya katika mchakato wa maridhiano ya kisiasa katika visiwa hivyo. Hatua hii inakuja baada ya vyama hivyo kusaini tamko la...
-
Kenya yatoa siku 90 kwa wageni wasio na vibali halali kuvitafuta
Serikali ya Kenya, imewatangazia raia wa kigeni wanaoishi nchini humo bila vibali vya kuishi au kufanya biashara, kuvitafuta ndani ya siku tisini.Hii inafuatia kauli ya rais William Ruto, wiki iliyopita, kuagiza operesheni dhidi ya wachuuzi wanaofanya biashara ndogo ndogo nchini humo. Je, hatua…
more -
Mpango wa rais Tshisekedi kuhusu mazungumzo yatafanikiwa ?
Mwishoni mwa mwezi wa Agosti, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, alitangaza mpango wa namna mazungumzo ya kitaifa yatakavyofanyika, kusaidia kuleta utulivu wa kisiasa nchini humo. Mazungumzo hayo yataanzia katika mikoa yote 26, kabla ya yale ya kitaifa kufanyika jijini...
-
DR Congo: Mvutano waendelea kuhusu mpango wa kuifanyia marekebisho katiba
Mahakama ya Katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwezi Julai, iliidhinisha sheria tata ya kufanyika kwa kura ya maoni, ili kuifanyia katiba mabadiliko baada ya kupitishwa na wabunge mwezi Juni. Hatua hii imewakera wapinzani wa rais Felix Tshisekedi, kutoka muungano wa C64 ambao…
more -
Kwanini kampeni za mapema zimeanza nchini Kenya, mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu ?
Ni mwaka mmoja, kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya. Uchaguzi huo utafanyika tarehe 10 mwezi Agosti mwaka 2027. Wakenya watamchagua rais, Magavana, Maseneta, wabunge, wawakilishi wa kike na viongozi wa Wadi mbalimbali. Hata hivyo, joto la kampeni ya mapema, imeshaanza kushuhudiwa, hasa kwenye...
-
Maridhiano ya kisiasa nchini Tanzania yatafanikiwa ?
Nchini Tanzania, maneno maridhiano na Katiba mpya, yameendelea kutawala vinywa vya wanasiasa na wananchi wa taifa hilo baada ya uchaguzi mkuu uliokumbwa na vurugu wa Oktoba mwaka 2025. Hivi karibuni, rais Samia Suluhu Hassan alikutana nna viongozi wa vyama vya siasa na kutangaza mpango wa...
-
Kenya: Je, Seneta Edwin Sifuna anataka kuwania urais 2027 ?
Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya 2027, nyota ya kisiasa ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna inaonekana kuanza kung'aa. Sifuna aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama cha ODM, sasa anaongoza vuguvugu linaloitwa Linda Mwananchi. Je, Sifuna ameanza kutembea kwenye viatu vya aliyekuwa kiongozi shupavu wa...
-
Je, mazungumzo ya kitaifa nchini DRC yatafanyika ?
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi amekubali kuanzisha mazungumzo ya kitaifa kujadili mivutano ya kisiasa likiwemo suala la kuibadilisha katiba na changamoto za kiusalama mashariki mwa nchi hiyo. Tayari muungano wa maaskofu wa kanisa katoliki CENCO na ule wa makanisa ya...
-
Kwanini vita vya Marekani na Iran vimeanza tena ?
Marekani na Iran zimeanza tena kushambuliana, na kuzua wasiwasi wa kuendelea kwa vita vilivyoanza mwezi Februari 2026. Mashambulizi haya yamelenga kudhibiti eneo la Bahari ya Hormuz, njia muhimu inayotumiwa na meli zinazosafirisha mafuta na gesi kuelekea katika maeneo mbalimbali ya dunia. Kwanini...
-
Rais Ndayishimiye ataweza kuleta maridhiano kati ya upinzani na serikali nchini DRC ?
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, wiki hii amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa upinzani kutoka muungano wa C64 na viongozi wa Kanisa Katoliki na Kiprotestanti nchini DRC, wanaopinga mchakato wa marekebisho ya katiba unaoungwa mkono na…
more -
Kwanini vita vinaendelea mwaka mmoja baada ya DRC na Rwanda kutia saini ya mkataba wa amani ?
Vita vimeendelea kushuhudiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kati ya wanajeshi na waasi wa M23/AFC wanaotuhumiwa kuungwa mkono na Rwanda licha ya Kigali na Kinshasa, kutia saini mkataba wa kusitisha vita mwaka mmoja uliopita. Kwanini vita vinaendelea licha ya kuwepo kwa mkataba…
more -
Serikali nchini Uganda inatumia Mahakama kuwanyanyasa wapinzani ?
Nchini Uganda, mwanasiasa wa upinzani na Meya wa zamani wa jiji la Kampala Erias Lukwago anakabiliwa na mashtaka ya uhaini. Alikamatwa nyumbani kwake na wanajeshi kwa agizo la Mkuu wa Majeshi Jenerali Muhoozi Kainerugaba na kuzuiwa kabla ya kufikishwa Mahakamani. Wiki hii, mwanasiasa mashuhuri na...
-
Kenya kuwalipa fidia waathiriwa wa maandamano ya kisiasa
Serikali ya Kenya, itaanza kuwalipa fidia watu karibu Elfu Mbili, walioathiriwa na visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwemo kuuawa, kubakwa, kutoweka na kujeruhiwa wakati wa maandamano ya kisiasa yaliyotokea nchini humo kati ya mwaka 2017 hadi 2025. Tume ya taifa ya haki za binadamu nchini...
-
Vijana nchini Kenya wanavyotumia teknolijia kuhamasisha elimu ya kisiasa
Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya mwaka 2027, vijana nchini humo, wanakumbatia teknolojia kuwafikia vijana wengi hasa wale wa rika la Gen Z, kujiandikisha kama wapiga kura na kuwania nyadhifa mbalimbali za uongozi. Je, hatua hii inaweza kuleta mwamko mpya wa kisiasa nchini Kenya ? Mwanahabari...
-
DR Congo: Wanasiasa wachuana kuhusu mchakato wa kuifanyia marekebisho katiba
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kumeundwa miungano miwili ya kisiasa. Kundi la kwanza linaitwa "C4" linalounga mkono mabadiliko ya katiba, chini ya rais Felix Tshisekedi. Nao vigogo wa upinzani wakiongozwa na Martin Fayulu, Moïse Katumbi na wengine, wao wameunda C64" vuguvugu linalopinga...
-
Kwanini kampeni za mapema zimeanza nchini Kenya kuelekea uchaguzi wa 2027?
Siasa za kampeni ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, zimeanza kupamba moto nchini Kenya, mwaka mmoja kabla ya wananchi kupiga kura. Rais mstaafu Uhuru Kenyatta amejitokeza waziwazi na kumkosoa mrithi wake William Ruto kwa namna anavyoongoza serikali. Ruto na washirika wake, wanamtaka Uhuru kuachana…
more -
Sheria mpya nchini Uganda yalenga vyama vya siasa vya upinzani
Nchini Uganda, rais Yoweri Museveni ambaye aliapishwa Mei tarehe 12 kuendelea kuongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano baada ya kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 40, ametia saini mswada tata unaolenga kudhibiti ushawishi wa kigeni nchini humo kuwa sheria. Ukiukwaji wa sheria hii...
-
Kwanini suala la siasa na usalama, halikupewa nafasi kubwa kwenye mkutano wa Afrika na Ufaransa ?
Mkutano wa siku mbili kati ya Ufaransa na mataifa ya Afrika, uliofanyika jijini Nairobi nchini Kenya kati ya Mei 11 hadi 12, haukutoa kipaumbele suala la siasa na usalama katika mataifa ya Afrika, wakati huu nchi kama DRC, Sudan na yale ya ukanda wa Sahel kama Mali, Niger na Burkina Faso...
-
Mpango wa DRC kuwakubali wahamiaji waliofukuzwa Marekani kwazua mjadala
Hatua ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kuingia kwenye makubaliano na Marekani ili kuwapokea wahamiaji haramu waliofukuzwa nchini humo, kumezua mjadala mzito katika nchi hiyo inayoendelea kukabiliwa na utovu wa usalama, hasa maeneo ya Mashariki. Kwanini kuna mvutano ?
-
Tanzania: Ripoti ya Tume imejibu maswali magumu kuhusu ukweli wa Oktoba 29 ?
Nchini Tanzania Aprili tarehe 23, tume iliyoundwa kuchunguza matukio ya vurugu yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka 2025, ilitoa ripoti yake. Kwa mujibu wa tume hiyo, watu zaidi ya 500 walipoteza maisha, maelfu walijeruhiwa huku uharibifu wa mali wenye zaidi ya thamani...
-
Kwanini Ruben Kigame, anataka kuwa rais wa Kenya 2027 ?
Uchaguzi Mkuu nchini Kenya ni mwezi Agosti mwaka 2027, lakini wanasiasa mbalimbali wameanza kuonesha nia ya kugombea kiti cha urais. Miongoni mwao ni Ruben Kigame, mwanasiasa, mwanaharakati, mhadhiri, mwandishi wa Habari na mwanamuziki maarufu wa nyimbo za Injili. Yeye ni mlemavu wa Macho…
more -
Mazungumzo mapya kati ya waasi wa M23/AFC na serikali ya DRC nchini Uswizi
Awamu ya tisa ya mazungumzo ya amani kati ya waasi wa M23/AFC na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yalianza siku ya Jumatatu Aprili 13 nchini Uswizi. Ujumbe wa Qatar ambao ni wasuluhishi, akiwemo mjumbe wa Marekani kuhusu masuala ya Afrika Massad Boulos, wanashiriki. Nini Ajenda ya...
-
Harakati za watetezi wa haki za binadamu Mashariki mwa DRC
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yakiongozwa na Amnesty International, katika ripoti zao, yamekuwa yakionya kuwa maisha ya wanaharakati wa haki za binadamu, wana habari na viongozi wa mashirika ya kiraia yapo hatarini katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa M23, Mashariki mwa DRC. Wiki hii...
-
Viongozi wa ODM wanaweza kuungana tena baada ya mpasuko wa chama ?
Chama siasa cha Orange Democratic Movement-ODM kinaendelea kugawanyika, kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2027 nchini Kenya. Tangu kufariki dunia kwa Raila Odinga, mwasisi wa chama hicho kikubwa cha upinzani, viongozi waandamizi wa ODM wameshindwa kuelewana kuhusu kuendelea kumuunga mkono rais William...
-
DR Congo: Ni wakati mwafaka wa kuibadilisha katiba ya DRC ?
Mjadala wa kuibadilisha katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, umepamba moto. Wanasiasa wanaoegemea upande wa rais Felix Tshisekedi na chama chake cha UDPS wanaunga mkono mchakato wa katiba kubadilishwa. Upinzani wakiongozwa na naibu Spika wa Bunge la Seneti aliyejiuzulu Modeste Bahati...
-
Nini hatima ya vita vya Marekani na Israeli nchini Iran ?
Ni wiki ya tatu sasa, baada ya Marekani na Israeli zilipoanza kutekeleza mashambulizi ya kijeshi nchini Iran. Mataifa hayo mawili yanasema lengo la mashambulizi hayo ni kuhakikisha kuwa inaharibu kabisa miundo mbinu ya Iran kutengeneza silaha za nyuklia. Rais wa Marekani Donald Trump, anasema…
more -
Kenya: Je, ushirikiano wa serikali kati ya vyama vya ODM na UDA unafanikiwa ?
Umepita mwaka mmoja tangu chama tawala nchini Kenya UDA na kile cha upinzani ODM, vilipoingia kwenye makubaliano ya kisiasa na kutaja mambo 10 kama vita dhidi ya ufisadi, kupunguza deni la taifa, ujumuishwaji ulio sawa serikalini kama baadhi ya mambo ya kushughulikia baada ya maandamano ya vijana...
-
Nini hatima ya vita vya Israel na Marekani nchini Iran ?
Dunia inashuhudia vita katika ukanda wa Mashariki ya Kati, baada ya Marekani na Israeli kuishambulia Iran, tangu Februari 28. Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu wanataka Iran iache kutengeneza silaha za maangamizi, kuyaunga mkono makundi yenye silaha nje ya...
We're indexing this podcast's transcripts for the first time — this can take a minute or two. We'll show results as soon as they're ready.
No matches for "" in this podcast's transcripts.
No topics indexed yet for this podcast.
Loading reviews...
ABOUT THIS SHOW
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
HOSTED BY
RFI Kiswahili
Loading similar podcasts...