Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii podcast artwork

PODCAST · news

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.

Publisher-supplied feed metadata · PodParley refreshed Jun 13, 2026 · Source feed

  1. 24

    Uchaguzi wa nchini Zambia, siasa za DRC, Kenya naTanzania kushika kasi

    Uchaguzi wa urais na wabunge ulivyofanyika nchini Zambia wiki hii, na sasa wananchi wanasubiri matokeo rasmi, baada ya vurugu za siku ya Ijumaa, rais wa Kenya William Ruto aliongoza mazungumzo kuhusu ruwaza ya Kenya 2060, muungano wa upinzani nchini DRC watishia kuitisha maandamano kupinga marekebisho ya katiba; tutaangazia siasa za Tanzania, Sudan, Washington kuiwekea vikwazo Iran kuhusu udhibiti wa mlango Bahari wa Hormuz.

  2. 23

    Mahakama ya haki yaratibu vikao vya kusikiliza kesi iliyowasilishwa na DRC dhidi ya Rwanda

    Mahakama ya Kimataifa ya Haki wiki hii iliratibu vikao vya kuskiliza kesi iliyowaislishwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo dhidi ya Rwanda, ambapo Kinshasa inaituhumu Kigali kwa kukiuka mikataba minne ya kimataifa ikiwemo mkataba wa mauaji ya kimbari, mkataba wa kupinga mateso na mkataba wa kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake.

  3. 22

    Kuzirai kwa kiongozi wa upinzani Uganda, mahakama ya katiba nchini DRC yaamua

    Kinara wa upinzani nchini Uganda azirai akiwa mahakamani, mahakama ya katiba nchini DRC ilisema kwamba sheria iliyopendekezwa kuhusu kuandaa kura ya maoni katika nchi hiyo ni ya kikatiba, seneta wa Nairobi Edwin Sifuna autikisa mwamba wa siasa nchini Kenya kuelekea uchaguzi wa 2027, siasa za Tanzania, Sudan, na Morocco ambako wahamiaji waliamua kuogelea kuvuka kwenda ulaya, uhispania, Washington ilisema mkataba wa kujisalimisha kwa Hamas kule Israeli umepatikana.

  4. 21

    Watu zaidi ya 20 kuuawa mashariki mwa DRC, mchakato wa katiba mpya Tanzania

    Shambulio la ADF laua zaidi ya 20 mashariki mwa DRC, ziara ya waziri mkuu Judith Suminwa huko Ituri, gavana wa zamani wa migori akutwa na hatia ya mauaji, huku rais Ruto akionya kuhusu matumizi ya wahuni kwenye mikutano ya kisiasa, siasa za Tanzania, Sudan na rais wa zamani wa Senegal Macky Sall, kuwasilisha maono yake mbele ya baraza la Umoja wa Mataifa, katibu mkuu wa UN Antonio Guteress atoa wito kwa pande zinazohusika katika mzozo wa mashariki ya kati kutafuta suluhu kupitia diplomasia.

  5. 20

    Matokeo ya uchaguzi mdogo Ol Kalou Kenya; rais wa DRC aitisha mazungumzo jumuishi

    Miongoni mwa yaliyojiri wiki hii ni wapiga kura na wanahabari walivyoshambuliwa wakati wa  uchaguzi mdogo Ol Kalau na kuzua hofu kuhusu uchaguzi wa 2027 nchini Kenya: wanafunzi wasiopungua 20 kupoteza maisha katika ajali ya barabarani kule Uganda, shambulio la waasi wa ADF huko Mangina mashariki mwa DRC, usalama kuzorota huko Sudan, ziara ya waziri mkuu wa Ufaransa Sebastien Lecornu kule Morocco, Trump aishutumu China kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani, na mengine zaidi.-

  6. 19

    Makubaliano kati ya Marekani na Iran kuvunjika, maandamano ya mawakili wa Kenya

    Yaliyojiri wiki hii ni kuvunjika kwa makubaliano kati ya Marekani na Iran, mazishi ya kiongozi wa kiroho wa Iran A.Khamenei, rais wa Tanzania Samia Suluhu kuwaonya wanaharakati dhidi ya kuchochea vurugu-wanasiasa wa upinzani, wanahabari pamoja na wanaharakati, Uganda waishi kwa hofu kutokana na vitisho vya mkuu wa majeshi, wapinzani wa jukwaa la C64 DRC walikutana na rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, na maandamano ya mawakili nchini Kenya

  7. 18

    DRC yasherehekea miaka 66 ya uhuru, amnesty yalaani vita Sudan, mazishi ya Khamenei huko Iran

    Makala imeangazia maadhimisho ya miaka 66 ya uhuru wa jamahuri ya kidemokrasia ya Congo, kuanzishwa kwa majaribio ya dawa zizonaweza kuwa tiba ya Ebola aina ya Bundibugyo huko DRC, kufungwa kwa kituo cha televisheni cha NTV na Gazeti la Daily Moniter nchini Uganda, shirika la Amnesty International, layatuhumu mataifa ya nje  kwa kuendelea kuchochea mzozo wa Sudan. Polisi nchini Afrika Kusini wazuia maandamano ya ghasia, utawala wa Tehran wakanusha kuomba mazungumzo na Marekani

  8. 17

    Maandamano ya Gen Z Kenya, ziara ya rais Ndayishimiye DRC,vifo Venezuela vyafikia920

    Maandamno ya vijana wa Gen Z kuwakumbuka wenzao waliouawa katika maandamano ya mwaka wa 2024 nchini Kenya, kesi ya aliyekuwa meya wa jiji la Kampala Uganda Erias Lukwago, ziara ya rais wa Burundi pia mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, jijini Kinshasa DRC, Evariste Ndayishimiye, yaliyojiri huko Sudan, Nigeria, Tunisia lakini pia mitetemeko miwili ya ardhi huko Venezuela iliyouwa watu zaidi ya 900, na pia kinachoendelea katika mlango bahari wa Hormuz kuhusu mkataba kati ya Irani na Marekani

  9. 16

    DRC na kombe la dunia, pia ebola,Gen z kuandamana juni 25 Kenya,hali ya sasa Iran

    Ni wiki ambayo imegubikwa na michuano ya kombe la dunia 2026 huko Marekani, wiki hii eneo hili la Afrika mashariki na kati lilichangamka baada ya timu ya DRC Leopards kutoka sare na Ureno, virusi vya ebola na juhudi za kikanda kuudhibiti, kukamatwa kwa wakili Erias Lukwago kule Kampala Uganda, lakini pia mashambulio ya kigaidi kwenye uwanja wa ndege wa mjini Niamey huko Niger, na mkutano wa G7 jijini Paris Ufaransa, na hali kadhalika kusainiwa kwa mkataba kati ya Marekani na Iran

  10. 15

    Michuano ya kombe la dunia, hali ya Ebola kwenye ukanda

    Ni wiki ambayo imegubikwa na maandamano kadhaa nchini huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, huko Nanyuki nchini Kenya, na watu kutoka nchi kadhaa za Afrika kuihama Afrika Kusini kutokana na ongezeko la chuki dhidi ya wageni, lakini kubwa kabisa wiki hii lililotikisa ulimwengu ni michuano ya kombe la dunia ya mwaka wa 2026 iliyong’oa nanga huko Marekani, Mexico na Canada, bila kuisahau ziara ya Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Leo wa Kumi na nne huko Uhispania.-Naitwa Ruben Lukumbuka, 

  11. 14

    Ufaransa yazindua mnara wa kumbukumbu ya genocide Rwanda, mgomo wa kitaifa DRC

    Ufaransa yazindua mnara wa ukumbusho wa mauaji ya kimbari huko Rwanda kwenye jiji la Paris, wapinzani wa DRC juni 03 waliitisha mgomo wa kitaifa, watu zaidi ya kumi waliuawa katika shambulio lililotekelezwa na waasi wa ADF huko Mbau wilaya ya Beni mashariki mwa DRC tunaangazia hotuba ya rais wa Uganda kwa taifa, ziara ya rais wa Tanzania huko Urusi, Afrika kusini kudai kuwa hakuna ubaguzi wala chuki dhidi ya wageni nchini mwake, hali ya Afrika magharibi, na mgogoro wa Ukraine na Urusi

  12. 13

    Wanafunzi 16 wafa katika moto wa shule ya bweni Kenya, mkuu wa WHO azuru DRC

    Wanafunzi kadhaa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika shule ya Sekondari ya wasichana Nakuru nchini Kenya, ziara ya mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO, Uganda kutangaza kuufunga mpaka wake na DRC, hali nchini Sudan, huku Nigeria, kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Januari mwaka ujao, na pia ripoti zinasema Marekani na Iran zakubaliana kuongeza usitishwaji wa vita kwa siku zingine 60

  13. 12

    DRC yashirikiana na WHO, AU kupambana na Ebola, sitisho la mgomo wa madereva Kenya

    Habari kuu za dunia wiki hii ni pamoja na kuzuka kwa mlipuko wa ugonjwa hatari wa ebola, DRC na juhudi za kimataifa zinazolenga kupambana na virusi hivyo, mkutano wa Kigali kuhusu nyuklia, mgomo wa madereva wa usafiri wa umma ulivyoathiri wananchi, Kenya, hali nchini Sudan ; lakini pia wahamiaji wasio na vibali wanavyohangaishwa kule Afrika kusini, ziara ya rais wa Urusi kule China ; lakini pia Marekani na Irani zikiendeleza vitisho kati yao

  14. 11

    Yoweri Museveni aapishwa muhula wa saba Uganda, kongamano la Afrika forward Nairobi

    Miongoni mwa habari kuu za dunia zilizopewa uzito juma hili ni pamoja na kuapishwa kwa rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa muhula wa saba, kufanyika na kutamatika kwa mkutano wa Afrika na Ufaransa jijini Nairobi nchini Kenya, kauli ya rais wa Rwanda Paul Kagame akikosoa vikwazo vya Marekani kuhusu nchi yake, eneo la Afrika magharibi hususan Nigeria, Ghana na Mali, lakini pia Ziara ya rais wa Marekani Donald Trump huko China. Ungana na Ruben Lukumbuka, kupata mengi zaidi

  15. 10

    Watu 518 walifariki Tanzania wakati wa vurugu za uchaguzi, mapigano bado yanaendelea DRC

    Taarifa kuu wiki hii ni ripoti ya tume ya uchunguzi nchini Tanzania iliyosema watu 518 walifariki wakati wa ghasia za uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka uliopita.  Tunaangazia pia taarifa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo licha makubaliano ya kusitisha vita kati ya waasi wa M23/AFC na serikali ya Kinshasa, kuendelea kushuhudiwa kwa mapigano ya mara kwa mara. Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Leo wa 14 alikamilisha ziara ya siku kumi barani Afrika juma hili; na katika mzozo wa Mashariki ya kati, Marekani yaongeza muda wa kusitisha mapigano na Iran, hatua sawa ikichukuliwa kati ya Israeli na Lebanon.

  16. 9

    Kifo tatanishi cha waziri wa habari wa Burundi, Iran na Marekani zatunishiana misuli

    Makala hii imeangazia kifo cha waziri wa mawasiliano na vyombo vya habari nchini Burundi Gabby Bugaga, waasi wa AFC/M23 na serikali ya DRC wanaokutana huko Uswis wakubaliana kuhusu kubadilishana na wafungwa, huku Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ikisisitizia msimamo wake wa kuitaka Rwanda kuwaondoa wanajeshi wake katika eneo la mashariki, ziara ya kiongozi wa kanisa katoliki nchini Cameroon kabla ya kuelekea Angola, na mvutano kati ya Iran na Marekani kuhusu mlango bahari wa Hormuz

  17. 8

    Rwanda yaadhimisha miaka 32, mauaji ya kimbari, Israeli yashambulia Lebanon

    Maadhimisho ya siku 100 maarufu kama kwibuka kukumbuka mauaji ya mwaka 1994 nchini Rwanda, mwanadiplomasia wa Marekani James Swan kuanza kazi kama mkuu wa Monusco huko DRC, mazungumzo kati ya serikali ya nchi hiyo na waasi wa M23 kufanyika kule Geneva Uswiz chini ya upatanishi wa Qatar, hali ya kisiasa nchini Kenya na Tanzania, na sudan; kampeni za uchaguzi mkuu nchini Benin kutamatishwa kuelekea siku ya jumapili ya aprili 12 na mashambulizi ya jeshi la Israeli huko Lebanon

  18. 7

    Waasi wa ADF waua 40 mashariki mwa DRC, Iran yapuuzi vitisho vya Trump

    Miongoni mwa matukio makubwa yaliyojiri wiki hii ni pamoja na timu ya taifa ya soka ya DRC Leopards kufuzu kushiriki fainali ya michuano ya kombe la dunia 2026, shambulio la waasi wa ADF laua 30 mashariki mwa DRC, watoto wanne wadungwa kisu hadi kufa katika shule moja nchini Uganda, wapigakura wahamasishwa kujiandikisha nchini Kenya na kupanda kwa bei ya mafuta, kuapishwa kwa rais wa Jamhuri ya afrika ya kati, vitisho vya Trump kuhusu mlango bahari wa Hormuz

  19. 6

    UN yasikitishwa na hali mashariki mwa DRC, miili 33 yagunduliwa nchini Kenya

    Miongoni mwa yaliyojiri wiki hii ni pamoja na baraza la usalama la umoja wa mataifa lataka kufunguliwa upya kwa viwanja vya ndege kwenye miji ya Goma na Bukavu mashariki mwa DRC, kiongozi wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine alisema uhuru wake sio mjadala, miili 14 ilipatikana iliyopatikana nchini Kenya kufanyiwa upasuaji kubaini chanzo cha vifo. utambuzi wa utumwa kuwa uhalifu dhidi ya haki za ubinadamu, na rais Trump, aahirisha mpango wake wa kushambulia vinu vya nishati vya Iran

  20. 5

    Bei ya mafuta yapanda duniani, DRC na Rwanda kupunguza uhasama

    Miongoni mwa matukio makubwa ni pamoja na mwendelezo wa mashambulizi ya Marelkani na Israeli huko Iran, na nchi za Ghuba, huku bei ya mafuta na gesi ikipanda, DRC na Rwanda zilikubaliana kupunguza uhasama wao, rais wa Kenya William Ruto alizindua ujenzi wa reli ya kisasa SGR katika eneo la magharibi mwa nchi yake, hali ya nchini Sudan na Senegal yavuliwa ubingwa AFCON, Morocco ilitangazwa mshindi. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka 

  21. 4

    Mashambulio yaendelea mashariki ya kati na mauaji ya mfanyakazi wa UNICEF DRC

    Makala hii imeangazia pakubwa mashambulio ya Marekani na Israeli huko Iran huku Irani nayo ikijibu mapigo kwa kuishambulia Israeli, na pia kuachiwa huru kwa aliyekuwa waziri mkuu wa Burundi Alain Bunyoni, shambulio la ndege zisizo na rubani lililowaua watu watatu miongoni mwao, mfanyakazi wa shirika la UNICEF kwenye mji wa Goma, mashariki mwa DRC, siasa za Kenya, Uganda na maeneo mengine ya Afrika.  

  22. 3

    Jeshi la Rwanda lawekewa vikwazo, Israeli na Marekani zashambulia Iran

    Matukio makubwa ya juma hili ni pamoja na Marekani kutangaza vikwazo dhidi ya  jeshi la Rwanda na maafisa wake wanne wakuu, Sudan iliishtumu Ethiopia kwa kuruhusu ndege zisizokuwa na rubani kuishambulia nchi yake mwezi februari na machi, Macky Sall rais wa zamani wa Senegal miongoni mwa wagombea watatu wanaotafuta ukatibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Marekani na Israel zimeendelea kutekeleza mashambulio mazito nchini Iran, huku Iran nayo ikijibu mapigo

  23. 2

    Msemaji wa waasi wa M23 aliuawa, Kenya yazindua dawa mpya ya Lenacapavir

    Matukio makubwa ya juma hili ni pamoja na kuuawa kwa msemaji wa kijeshi wa kundi la waasi la M23 Willy Ngoma, serikali ya Kenya ilizindua zoezi la usambazaji wa dawa ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi, LENACAPAVIR, UN ulisema taifa la Sudan Kusini, linatoa hifadhi kwa wakimbizi zaidi elfu 64, watu 25 waliuawa katika jimbo la Adamawa, kaskazini mashariki mwa Nigeria, pia awamu ya tatu ya mazungumzo ya kidiplomasia kuhusu mradi wa Nyuklia wa Iran, yalifanyika juma hili huko  Geneva Uswiz

  24. 1

    Ndayishimiye ndiye mwenyekiti mpya wa AU, ujumbe wa EU wazuru mashariki ya DRC

    Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye achaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika (AU) mwaka 2026, ziara ya ujumbe wa Umoja wa Ulaya huko DRC, vijana wa Afrika  wahadaiwa kupewa kazi nzuri Urusi, na kulazimishwa kupigana vita Ukraine, raia 18 wa Senegal na mmoja kutoka Ufaransa wahukumiwa kwa kuzua  fujo wakati wa mechi ya fainali  AFCON  jijini Rabat. Mkutano wa kimataifa kati ya India na Ufaransa kuhusu akili mnemba, pia tishio la Trump kuishambulia Iran

Type above to search every episode's transcript for a word or phrase. Matches are scoped to this podcast.

Searching…

We're indexing this podcast's transcripts for the first time — this can take a minute or two. We'll show results as soon as they're ready.

No matches for "" in this podcast's transcripts.

Showing of matches

TOPICS IN THIS SHOW

Click any topic to search every transcript on PodParley for moments someone mentioned it.

Loading reviews...

ABOUT THIS SHOW

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.

HOSTED BY

RFI Kiswahili

Produced by France Médias Monde

CATEGORIES

Frequently Asked Questions

How many episodes does Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii have?

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii currently has 24 episodes available on PodParley. New episodes are automatically indexed when they're published to the podcast feed.

What is Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii about?

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.

How often does Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii release new episodes?

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii has 24 episodes. Check the episode list to see recent publication dates and frequency.

Where can I listen to Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii?

You can listen to Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii on PodParley by clicking any episode. We provide an embedded audio player for direct listening, and you can also subscribe via your preferred podcast app using the RSS feed.

Who hosts Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii?

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii is created and hosted by RFI Kiswahili.
URL copied to clipboard!